Mbunge wa Chama cha ODM, Charles Were apigwa risasi na kuuawa

Mbunge wa Chama cha ODM, Charles Were apigwa risasi na kuuawa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Mbunge wa Chama cha ODM, Charles Were amepigwa risasi na kuuawa katika mzunguko wa hifadhi ya City kwenye barabara ya Ngong jijini Nairobi na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki muda mfupi uliopita.

Were ni mbunge wa Chama cha ODM wa eneo bunge la Kasipul.

Tukio kama la shambulio la Tundu Lisu 2017

Screenshot 2025-05-01 021644.png


Maafisa usalama nchini Kenya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye eneo la hifadhi ya City kwenye barabara ya Ngong jijini Nairobi, sehemu aliyopigwa risasi, Mbunge wa Chama cha ODM, Charles Were, wakikagua gari alilokuwemo Mbunge huyo baada ya kupigwa risasi na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki.
 
Mbunge Charles ameshambuliwa kwa risasi na watu wawili wasiojulikana waliokuwa kwenye Bodaboda na kupoteza Marsha

Dereva wa mbunge Huyo amenusurika katika shambulio Hilo lililotokea Nairobi

Source: Citizen tv

Tukio kama la shambulio la Tundu Lisu 2017
Dadeq tayari uko bwaxi hapo kupoteza Marsha ndiyo nini hicho,hizi pombe za offer zitakuua wewe dogo.
 
Were ni mbunge wa Chama cha ODM wa eneo bunge la Kasipul.

Mbunge Charles Ong'ondo Were wa Eneo bunge la Kasipul lipo katika kaunti ya Homa Bay iliyopo magharibi (western) nchini Kenya.

Mbunge huyo alishambuliwa kwa risasi barabara ya Ngong Road ambayo ni barabara kuu tajwa yenye magari mengi inayotoka CBD (mjini kati) ya Nairobi kuelekea hadi Ngong Town majira ya saa moja jioni akitokea kwenye shughuli za Bungeni mjini Nairobi

Watu wa karibu wanasema marehemu Charles Ong'ondo Were alishaifahamisha Ofisi ya DCI ( Ofisi ya mkurugezi wa upelelezi) kwamba maisha yake yapo hatarini.
 
No election No reform, jamaa wana katiba mpyaaaa, na maandamano yao kila siku na yanalindwa na polisi wengi tu
Kweli jamaa wapo huru
 
Mbunge wa Chama cha ODM, Charles Were amepigwa risasi na kuuawa katika mzunguko wa hifadhi ya City kwenye barabara ya Ngong jijini Nairobi na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki muda mfupi uliopita.

Were ni mbunge wa Chama cha ODM wa eneo bunge la Kasipul.

Tukio kama la shambulio la Tundu Lisu 2017

View attachment 3321294

Maafisa usalama nchini Kenya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye eneo la hifadhi ya City kwenye barabara ya Ngong jijini Nairobi, sehemu aliyopigwa risasi, Mbunge wa Chama cha ODM, Charles Were, wakikagua gari alilokuwemo Mbunge huyo baada ya kupigwa risasi na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki.
View attachment 3321298​
Kenya hawecheki na wowote 🤨
 
Back
Top Bottom