PreGE2025 Mbunge wa COVID 19, Anatropia asema no reforms no election ndio msimamo wa mwanademokrasia yeyote hata wana CCM

PreGE2025 Mbunge wa COVID 19, Anatropia asema no reforms no election ndio msimamo wa mwanademokrasia yeyote hata wana CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
"Waliotafuta majukwa mengine nawapongeza lakini mimi ni mmoja ya wabunge hawa wanaoitwa 'Covid 19' niliyeandika barua ya kuomba kurudi kwenye chama kwahiyo bado naamini CHADEMA ndiyo jukwaa sahihi pamoja na yaliyotokea nimeomba kupata nafasi nyingine kwenye chama"

"Nilichokuwa nakipigania kabla bado kipo nilichokuwa nakisemea hakijabadilika bado mimi ni mmoja ya watu ninao amini ili Serikali iliyopo madarakani ifanye vizuri inahitaji upande wa kuishauri hatuwezi kuwa ni watu wa kusifiana tu ooh tunaupiga mwingi tunaupiga mwingi"

"Nimekuja kumuunga mkono Mwenyekiti (Tundu Lissu) anachopitia kwasababu naamini anachopigania ndicho ambacho nimekuwa nikikipigania mimi pengine ningekuwa kwenye fursa kama ya kwake pengine ningekuwa kwenye mazingira sawa na anachopitia 'no reforms no election'ndio msimamo wa mwanademokrasia yeyote hata wana CCM"- alisema Anatropia Theonest, jana akiwa Mahakamani Kisutu katika kesi ya Tundu Lissu, Mwenyekiti CHADEMA Taifa.
1751463203651.png


Chanzo Nipashe
 
Back
Top Bottom