Pre GE2025 Mbunge wa Itilima asema alijiunga CCM baada ya Mzee Manyoni kugushi saini yake, CCM wanazidi kuuthibitishia umma huwa wanafanya umafia kwenye uchaguzi

Pre GE2025 Mbunge wa Itilima asema alijiunga CCM baada ya Mzee Manyoni kugushi saini yake, CCM wanazidi kuuthibitishia umma huwa wanafanya umafia kwenye uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mbunge wa Itilima amesesema alijiunga CCM baada ya Mzee Manyoni ambaye kwa sasa ni katibu wilaya ya Itilima kugushi saini yake,

CCM wanazidi kuuthibitishia umma huwa wanafanya umafia kwenye uchaguzi hapa wanaonesha kuwa huo ndio utamaduni wao.

Hata kura feki ambazo huwa zinakamatwa kipindi cha uchaguzi wanaonesha kuhusika kwa asilimia zote kutengeneza kura hizo ili kushinda kiwiziwizi.

Hili linathibitika ambapo mbunge wa jimbo hilo akieleza alipokuwa anajiunga na chama hicho kwa njia za kugushi.

Haya yanajiri katika mkutano Mkuu Maalum Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Itilima, mkoani Simiyu Februari 15, 2025 ambapo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akiwa ni mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu huo.

Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

 
Back
Top Bottom