Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga atimiza ahadi ya kampeni kwa kukabidhi "dustbin" mbili Zahanati ya Kijiji cha Kaning'ombe

Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga atimiza ahadi ya kampeni kwa kukabidhi "dustbin" mbili Zahanati ya Kijiji cha Kaning'ombe

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Mlipokuwa mnaambiwa kwamba wapinzani wanachelewesha maendeleo haikuwa masihara, yale yalikuwa ni magunzi katikati ya betri za tochi.

Huko jimbo la Kalenga mbunge Kiswaga ametimiza ahadi yake ya kutoa Dustbins mbili (2) kwenye zahanati na baada ya tukio hilo la kihistoria, picha ya pamoja ilipigwa huku mwananchi mmoja kwa furaha akitoa ishara ya dole gumba akimaanisha mambo ni fayaaaa.

Hongera sana Mbunge. Endelea kuchapa kazi babaaa!

Tunatarajia kuendelea kuona press releases nyingi za CCM kama hizi wakati ukiwa unaendelea kutumiza ahadi zako, hao ushamalizana nao hawakudai kura zao hazikupotea bure. On to the next one, please!

Screen Shot 2021-01-18 at 3.28.12 PM.png
 
hujasema uongo ndugu yetu,mheshimiwa kiswaga ni muungwana aliwaahidi dust bins 2 wakampa kura na katimiza ahadi,ni maendeleo uchafu utakuwa hautupwi hovyohovyo tena
Mkuu mpaka karne hii huku kusini kwa jangwa la sahara bado tunazungumzia swala la kutupa takataka hovyo na kuziweka mahali sahihi nayo ni maendeleo.

Nchi ya uchumi wa kati kazi tunayo.
 
Mkuu mpaka karne hii huku kusini kwa jangwa la sahara bado tunazungumzia swala la kutupa takataka hovyo na kuziweka mahali sahihi nayo ni maendeleao
Nchi ya uchumi wa kati kazi tunayo
Hawa ni watawala mkuu siyo viongozi
 
Kama wananchi wake wameridhika na wana amani, wewe ni nani unaemzodoa Mbunge?
 
Hahaaaa...
Pumbaaav!

"Tumeahidiiii.....Tunatekeleza"

Leta dustbin nyingine 3 tutekeleze ilani ya CCM yenye kurasa 303😂
 
Back
Top Bottom