Tetesi: Mbunge wa Jimbo la Msalala adaiwa kugawa ng'ombe wawili kila kijiji

Sawa tuu nyie endeleeni kupiga Domo la DP World 😁😁

Harafu Kwa taarifa Yako Rais alitoa hao Ng'ombe sio huko Msalala tuu na maeneo mengine mengi tuu.
 
Unaacha kujadili hatari ya 'kimarinda' inayomkabili 'raisi' wenu lissu huko ulaya anakokimbilia kila mara we unajadili habari za ng'ombe wanaouzika hadi 200,000/=
 
Too low ya ufikiri. Hapo umeona kwa upeo huo ni mboga tu. No kuna zaidi ya hilo uliloona, ndio la kujadili sasa.
Unasoma tu uzushi kutoka kwenye JF, na hufahamu background ya anayetuhumiwa na unaamini kibwege tu!!

Huu ni undezi
 
Hajadili mboga anajadili rushwa waliopewa wabunge ili wao na wananchi waunge mkono biashara ya bandari, ukitaka ufanikiwe wahonge wananchi kupitia wabunge wao.
Weka picha basi angalao ya huyo mbunge akipokea rushwa au akigawa ng'ombe!! Mnadandia kila uwongo mnaopewa na wazushi.
 
Hakuna mashaka yoyote kuwa wabunge walihongwa, wanahabari akina Kitenge walihongwa, na kuna mazingira yanayoashiria kuwa hata baadhi ya viongozi wa serikali waliotengeneza hili deal liosababishwa wabunge wahongwe, wao walihongwa zaidi.

Na kampuni ya DP ina sifa mbaya katika uadilifu. Ilifanya vivyo hivyo kwa viongozi wa serikali ya Djibout.

Tungekuwa na taasisi zilizo huru za kushugjulikia masuala ya rushwa na uadilifu, tayari kuna watu wangekuwa korokoroni. Lakini bahati mbaya sana, Serikali yenyewe imejaa wala rushwa, TAKUKURU imejaa wala rushwa, wanaoitwa wabunge, tangu kupatikana kwao huwa kunahusha michakato iliyojaa rushwa. Hivyo hakuna wa kumkamata mla rushwa na mtoaji rushwa.
 
Kwanza kabisa tunatakiwa kuwafundisha watu wetu kwamba hatuchagui wabunge ili watupe zawadi au watumie pesa zao binafsi kufanya kazi za uma.
Kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananchi, kushiriki kutunga sheria zenye manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla, kusahihisha na kupitisha mipango ya mapato na matumizi ya serikali, ..., ....
Kuisimamia na kuiwajibisha serikali inapoenda kinyume na matarajio ya wananchi.
Hatuhitaji wabunge wanaogawa pesa zao au kuzitumia kwa kazi za uma kama njia ya kutafuta kukubalika au kuchaguliwa tena.
Kosa kubwa ni kuhusisha ubunge na pesa. Matatizo ya sheria mbovu, mikataba mibovu, bajeti zisizo halisi, wabunge wajinga...... ndiyo matokeo yake.
 
Ujumbe kuntu kwa wahusika 🙏🙏
 
Miongoni mwa akili za ajabu ni hizi,angetoa MO au BAKH ungewapongeza,kutoa ni moyo tuache ulimbukeni ,MB kafanya kazi nzuri sana sana apongezwe Kwa kutoa msaada .
 
Huyu amaefanya vyema shibe Ni muhumu mno ,nchi hi ngumu sna Ni namba mbili kwa idadi ya mifugo duniani ila ajabu watu wake kula nyama Ni kwa mbinde mno

Kuna siku niliropoka kwa jirani yangu kuwa mm huwa nanuna kilo 3 za nyama naweka ktk friji ,,jirani aliona Ni hatari mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…