joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Sio kweli hayo unayosema, katiba yetu hii tunayoitumia sasa ilitungwa mwaka 1977, na kuanzia kipindi chote hich hadi leo Tanzania imeiacha kwa mbali sana Kenya katika kipengele cha demokrasia kwa viwango vya kimataifa(www.rsf.org), tangu dunia hii imeundwa hakuna hata mwaka mmoja ambapo takwimu za kimataifa zinaonyesha kwamba Kenya imeipita Tanzania katika demokrasia, hata baada ya Kenya kupata katiba mpya hiyo unayoisema inatoa demokrasia 2010, jaribu kupitia hiyo website niliyokupa hapo juu urudi miaka kumi nyuma utagundua huu ukweli ninaokuambia, ni kweli kwamba Magufuli anabinya kipengele cha freedom of political expression, lakini bado Tanzania ina uhuru zaidi katika maeneo mengine kuliko Kenya.Kama Kuna kitu Wakenya wanachukia ni rais aliye na nguvu nyingi. Magufuli ni dictator na japo Wakenya wanampenda kwa kupunguza ufisadi, Wakenya hawawezi kuvumilia udikteta wa kukandamiza viombo vya habari na udikteta mwingi tu aliyonayo. Ana nguvu kupita kiasi na ndio maana T.Z mna Katiba useless kabisa na nyinyi mnashughulikiwa kama mahabusu. Hamuezi ongea, Hamuezi jitetea. Hata Chadema haikuenda mahakamani kwa sababu ya Katiba yenu iliyo na udikteta. Katiba yenu haiwatambui kama watu wenye haki bali kama mahabusu ambao hawaezi kujieleza. Hamna freedom of expression.
Kuhusu Kenya kuchukia zaidi kukosa uhuru wa kujieleza kuliko wanavyochukia Ukabila, rushwa, insecurity, kutokuwapo na usawa katika umilikaji wa ardhi, na kuwa na pengo kubwa kati ya matajiri na masikini, hilo ni chaguo la wakenya, hatuwezi kuwaingilia, ila sidhani kama wakenya wengi watakubaliana na wewe.
Kuhusu wapinzani kutokwenda mahakamani sio kwa sababu ya katiba, kumbuka hata NASA walishasema hawatoenda mahakamani kwa kuona kwamba wasingetendewa haki wakichukulia mfano wa hukumu ya uchaguzi wa mwaka 2013, walihisi hawakutendewa haki, sasa mbona Jubilee wanalalamika baada ya NASA kutumia haki yao ya kikatiba na mahakama kufanya kazi yake waliyopewa kwa mujibu wa katiba ya nchi?, tuseme hapo katiba ndiyo mbaya au ni watu kukosa imani na mahakama?