Mbunge wa Jubilee awasilisha muswada Mahakama ya Juu kumuondoa Jaji David Maraga aliyefuta matokeo ya Urais

Sio kweli hayo unayosema, katiba yetu hii tunayoitumia sasa ilitungwa mwaka 1977, na kuanzia kipindi chote hich hadi leo Tanzania imeiacha kwa mbali sana Kenya katika kipengele cha demokrasia kwa viwango vya kimataifa(www.rsf.org), tangu dunia hii imeundwa hakuna hata mwaka mmoja ambapo takwimu za kimataifa zinaonyesha kwamba Kenya imeipita Tanzania katika demokrasia, hata baada ya Kenya kupata katiba mpya hiyo unayoisema inatoa demokrasia 2010, jaribu kupitia hiyo website niliyokupa hapo juu urudi miaka kumi nyuma utagundua huu ukweli ninaokuambia, ni kweli kwamba Magufuli anabinya kipengele cha freedom of political expression, lakini bado Tanzania ina uhuru zaidi katika maeneo mengine kuliko Kenya.

Kuhusu Kenya kuchukia zaidi kukosa uhuru wa kujieleza kuliko wanavyochukia Ukabila, rushwa, insecurity, kutokuwapo na usawa katika umilikaji wa ardhi, na kuwa na pengo kubwa kati ya matajiri na masikini, hilo ni chaguo la wakenya, hatuwezi kuwaingilia, ila sidhani kama wakenya wengi watakubaliana na wewe.

Kuhusu wapinzani kutokwenda mahakamani sio kwa sababu ya katiba, kumbuka hata NASA walishasema hawatoenda mahakamani kwa kuona kwamba wasingetendewa haki wakichukulia mfano wa hukumu ya uchaguzi wa mwaka 2013, walihisi hawakutendewa haki, sasa mbona Jubilee wanalalamika baada ya NASA kutumia haki yao ya kikatiba na mahakama kufanya kazi yake waliyopewa kwa mujibu wa katiba ya nchi?, tuseme hapo katiba ndiyo mbaya au ni watu kukosa imani na mahakama?
 
pengo lamasikini ni lazima na hata kwa bibilia yalikuwepo toka zaman. kenya wapo juu. watz, wengi tunataman sana kuwa wa kenya
Wewe ni maoni yako na hujazuiwa kwenda Kenya, na kuna wakenya wengi zaidi wanaotamani kuja Tanzania kuchangamkia fursa nyingi ambazo wewe huzioni, kuthibitisha hilo ni pale wakenya na serikali yao wanavyolalamikia serikali ya Tanzania kwa kuweka vikwazo kwa watu wengine wa nchi za EAC kuja Tanzania, wasingetamani kuja Tanzania wasingelalamika, Ethiopia imeweka vikwazo zaidi ya Tanzania lakini wakenya hawalalamikii Ethiopia kama wafanyavyo kwa Tanzania, jibu ni kwamba Tanzania ina fursa nyingi zaidi kuliko nchi zingine, wewe endelea kulalamika
 
Huu ni ujinga wa hali ya juu.If we keep up this corrosive culture of removing judges ,removing IEBC commissioners ,removing EACC heads ...believe me we will never achieve mature,professional and unduly influenced institutions.And this corrupting culture is coming from both sides of the political divide
 
katiba ya Kenya ilimtoa rais kabisa kwenye sector ya judiciary so the Kenyan president hana power ya kuteua au kumfuta kazi judge yeyote...rais hausiki kabisa kwenye idara ya judiciary, hiyo ni kazi ya judicial service commission
Na Judicial Service Commission hupatikana vipi kwa mujibu wa Katiba ya Kenya? Hv sio wateule wa Rais wale!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwani Tanzania amna Mauaji akiri kisoda
 
Jubilee wanazidi kuleta aibu kila kuchao, ilihali hawajafanya chochote cha kusuruhisha matatizo ya vijana walio wengi napenda maendeleo ya jubilee lakini wakati huu mtanisamehe , sababu kura yangu hampati mara ya pili na simanishi nitawapa wapinzani lakini hio siku nitapumzisha mwili wangu nyumbani
 
Kwani Tanzania amna Mauaji akiri kisoda
Hakuna nchi isiyo na mauaji, ndiyo maana zimepangwa kwa madaraja, ukilinganisha Kenya na Tanzania katika mauji holela, Kenya ipo kiwango cha PhD na Tanzania ndiyo ipo mwaka wa kwanza kupata digirii ya kwanza
 
true dat
 
Hakuna nchi isiyo na mauaji, ndiyo maana zimepangwa kwa madaraja, ukilinganisha Kenya na Tanzania katika mauji holela, Kenya ipo kiwango cha PhD na Tanzania ndiyo ipo mwaka wa kwanza kupata digirii ya kwanza
Kwa mkondo mnaochukua mbona msifike tu? Hivi karibuni tz ndo mtakuwa mna PhD tatu tutaanza kuja darasani huko kwenu!
 
Utakuwa umefanya jambo lisilo la hekima jombaa, we siku ya kupiga kura amka mapema maliza jukumu lako kwa nchi yako afu nenda kapumzike. Tupia U.Kenyatta kura aisee we mwenyewe si unaona alivyo jaribu hiyo miaka minne?
 
Kwa mkondo mnaochukua mbona msifike tu? Hivi karibuni tz ndo mtakuwa mna PhD tatu tutaanza kuja darasani huko kwenu!
Sijambo la kulipinga hilo, kama hali itaendelea hivi hivi ilivyo tunaweza kuwafikia Kenya, ila lakushanga sijui Kenya hawapendi tuwafikie?, kwasabu wanaongeza kasi kila uchao[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Sasa io petition inahusiana vipi na jubilee?
 
Na wewe huoni mapungufu ya hoja yako ambapo una upotevu zaidi.Ni vizuri Kenya tumeweka nguvu kwa tume ambapo kuna "panel of experts" kuamua nani anayefaa kwa kazi tofauti yaani we invest in institutions not individuals.Hata Obama alipozuru Ghana alisema "Africa should invest in istitutions and not strongmen" sababu madikteta ndio wameharibu Afrika zaidi na uamuzi mbaya,utawala mbaya na kutojali au kujenga "rule of law" .Strongmen don't last ,but good decisions made by healthy institutions have a lasting legacy.
 
Katiba nzuri ni ile inayotoa ufumbuzi wa matatizo yanayowakumba wananchi wa kawaida, ni ile ambayo itamuinua wananchi walio wengi hasa wale masikini. Matatizo ya msingi yanayozikabili jamii zetu hizi za afrika ni umasikini, ukosefu wa ajira, uhakika wa chakula, usalama, rushwa, matumizi mabaya ya fedha za uma na uzembe na matumizi mabaya ya ofisi za umma, hayo ndiyo hasa tunataka yapatiwe ufumbuzi kwamba, kabla hata hayo mambo ya kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani, kwani hayo hayana tija ya moja kwa moja kwa mwananchi wa chini.

Kinachojitokeza ni kwamba katiba ya Kenya imelenga zaidi kuwasaidia wanasiasa wasidhulimiwe kura zao, kuliko kutoa ufumbuzi wa matatizo ya wananchi wa chini masikini, kwa sababu tangu katiba hii ipatikane takribani miaka saba sasa hivi, rushwa ndiyo imeongezeka zaidi, ukosefu wa ajira ndiyo unazidi, usalama nchini ndiyo unazidi kuzorota, ugumu wa maisha ndiyo usisemi kitu, ukabila unakita mizizi, yaani yale matatizo ya wakenya masikini ndiyo yanaongezeka, lakini utasikia watu wakiisifia katiba, kwa sababu tu inatoa fursa nzuri kwa wanasiasa kufanya siasa wakiwa huru zaidi, basi katiba hii ni nzuri kwa wanasiasa lakini haimsaidii mwananchi wa kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…