Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machalli avamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana!

Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machalli avamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana!

Hiyo itakua ilipangwa ili asiwe bungeni wakati taarifa ya serikali kuhusu gharama za visimbusi inawakilishwa asikuwepo kuhoji.Spika anatoa report ati kaavamiwa na majambazi,mmmm CCM wamekua majambazi sasa
CCM = Chama Cha M........... ulikuwa hujui tu!.
 
Kikosi cha mauaji kutoka Lumumba watakuja na majibu mepesi kuwa alivamiwa na VIBAKA au WAHUNI Wa Dodoma. Tanzania zaidi ya uijuavyo.
 
pole sana MOSES Mungu ni mwema utapona tu! nadhani utekelezaji wa kauli ya serikali kupitia kwa waziri mkuu imeanza kufanyiwa kazi
 
Pale uliposema Chadomo na ccm vifutwe ndipo palikuponza, hawa kina Idd amin Dada huwa hawapendi na uliona mitusi ilivyomiminika kutoka kwa babavichaa.....we ungesema ccm kifutwe ungeona wingi wa pongezi na wala hayo yasingekukuta....Ila Mungu akupe nafuu mapema urudi kwenye mapambano, babavichaa watashughulikiwa na dunia na mwisho wao upo karibu.
 
[h=5]“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka.”[/h]
 
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka.”

Mkuu,

Kitufe cha like sikioni. Asante sana.

W/Mkuu amefungulia green guard/police kupiga watu. Kichapo sasa nimbadala wa sheria.
 
kuna vijana w green guard wanafundishwa technic za kupiga na kujeruhi watu ,wako mbeya na sasa ndo kipindi cha kufanya practical au field training wamegawanywa sehemu mbalimbali za nchi,KAMA WAO WAMEFUNDISHWA KUPIGA NA SS TUTAJIFUNZA KUPIGWA.
 
Mkuu,
Wewe ni mtu mwenye heshima sana hata kama unatumia ID nyingi. Kupotosha mambo kwa makusudi kwa staili hii kunakupunguzia heshima na credibility. Hiyo kauli machali hakuitoa, vinginevyo niletee hansard ya Bunge.
Heshima yoyote wewe ndiyo unayempa kichwa aonekane ana heshima,watu wengine waliisha mgundua siku nyingi.
 
Huyu bwana mdogo machali ni kilaza wa nguvu, kasulu hawataki hatakumwona na ameshahamishia makaz yake dom akihofia usalama wake, sasa na dom wameanza kumshushia vipigo, namshauri abadilike aanze kutetea wananchi na sio kuwapuuza na kuishambulia cdm
 
Liwalo na liwe,,,,,kung fu ni muhimu kwa wabunge wote,,,,for self defence,,unaona sasa machali,,,ukipona hoja binafsi,,,maana ha ha ha ha wapigwe tu,,na watapigwa
 
JUNE 20, 2013

Mbunge wa kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mh. Moses Machalli

Habari zilizoifikia Maisha Times muda huu kutoka Dodoma zinaripoti kwamba Mbunge wa Kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mh. Moses Machalli amevamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana katika eneo la, tukio hilo limetokea jioni hii wakati Mh. Machalli akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita kitendo ambacho kilionekana kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni hali iliyopelekea vijana hao kumtolea matusi kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa hasira ndipo kipigo kikali kilipoanzia.

Shuhuda wetu aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema kwamba Mh. Machalli amepigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.

Maisha Times itazidi kukuhabarisha zaidi kuhusiana na tukio hili kadiri habari zitakavyozidi kupatikana.

Imechapishwa na Mkamis

Wametumwa na mfipa hao. Sasa ameanza kuonyesha rangi yake halisi baada ya kuvaa ngozi ya kondoo kwa miaka mingi.
 
Tuanze na wenye mgogoro na bwana Machali ili tuweze kuwabaini mapema wahusika wa hilo tukio.

Kumbukumbu zangu; mchango wa mwisho wa bwana Machali bungeni ulikuwa ukiitaka serikali ichunguze suala la Arusha, na kama CHADEMA ikibainika imehusika basi kifutwe haraka sana.

Je, CHADEMA na kichapo alichopata Machali vina mahusiano?

We wa kike ama wa kiume? Unakua na Maneno ya uongo mbona? wote tulimsikia alisema ''Kwa vile CCM na CDM wanatupiana mpira! Kwa nini Msajiri asivifute vyama hivi?'' mbona CCM hujaihusisha? Unagongwa nini?
 
Back
Top Bottom