SI KWELI Mbunge wa Kaunti ya Tongaren, John Chikati ashambuliwa na waandamanaji kwenye Maandamano ya Gen Z Kenya

SI KWELI Mbunge wa Kaunti ya Tongaren, John Chikati ashambuliwa na waandamanaji kwenye Maandamano ya Gen Z Kenya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
GQ7NJMUXEAAKwG0.jpg
Inadaiwa kuwa picha hii inamuonesha Mbunge wa Kaunti ya Tongaren Kenya, John Murumba Chikati akiwa amevamiwa na kushambuliwa na wananchi baada ya kupigia kura ya ndiyo Muswada mpya wa Sheria ya fedha.
 
Tunachokijua
Kutokana na kutokuridhishwa na mapendekezo ya Kuongeza kodi na tozo kwenye Muswada mpya wa Sheria za Fedha nchini Kenya, vijana wa nchi hiyo maarufu kama Gen Z waliamua kuazisha maandamano kama sehemu ya kufikisha malalamiko yao kwa mamlaka ziweze kuchukua hatua ili kupunguza ukali wa maisha.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Taarifa ya Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya (KNCHR), hadi kufikia Julai 2, 2024, takriban watu 39 wamepoteza maisha kutokana na Maandamano hayo yaliyodumu kwa zaidi ya wiki moja huku wengine 361 wakijeruhiwa.

Pamoja na mambo mengine, maandamano haya yameshuhudia matukio mengi ya kusisimua ikiwemo waandamanaji kuvamia Bunge pamoja na kula vyakula vya wabunge kwenye kantini yao.

Madai ya kushabuliwa kwa Mbunge Chikati
Juni 25, 2024, taaarifa za waandamanaji kumshambulia MBunge wa Tongaren, John Chikati Murumba zilianza kusambaa Mtandaoni.

Mathalani, Mtumiaji wa mtandao wa X anayefahamika kwa jina la Omwamba aliweka picha ya mtu aliyejeruhiwa anayetajwa kuwa Chikati yenye ujumbe unaosema "Tongaren MP John Chikati Murumba who Voted yes for the Finance Bill 2024 amesalamiwa kidogo na wananchi"

Hata hivyo, ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini picha hiyo si ya John Chikati kama inayodaiwa. Kupitia utafutaji wa kimtandao kwa kutumia Google Image Search, JamiiCheck imebaini kuwa anayeonekana kwenye picha ni Francis Mwijukye, Mbunge kwa kaunti ya Buhweju nchini Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Polisi, Mwijukye alishambuliwa na wananchi Juni 12, 2024 wakati akitatua Mgogoro wa ardhi jimboni kwake.

"Mbunge alipokea malalamiko kutoka kwa waumini wa Kanisa Katoliki la Rwanyamabare na wanachama wengine wa Chama cha Wakulima cha Rwamabare, ambao walidai kwamba kanisa lao liko katika hatari ya kuondolewa/kubomolewa na Kamugisha Frank, jirani ambaye wana mgogoro naye juu ya ardhi ya kanisa hilo. Wakati wa tukio hilo, Mhe. Mbunge alikabiliana na kundi hasimu, waliokuwa na fimbo. Wakati wa mapambano ya vurugu, Mhe. Mbunge alipata majeraha mabaya kichwani na alikimbizwa na polisi katika Kituo cha Afya cha Nsiika 4 kwa matibabu" inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Baadhi ya vyombo vya habari vya Uganda vimeripoti pia kuhusu kadhia aliyopitia mbunge huyu. Rejea hapa, hapa na hapa.

Pamoja na kuchunguza suala hili, tarifa ya Polisi iliukumbusha Umma kujua kwamba wabunge ni wawakilishi wa wapiga kura wao na wanabeba jukumu la Bunge hivyo vitisho vyovyote vya vurugu dhidi ya wabunge ni shambulio dhidi ya msingi wa demokrasia na wanaofanya hivyo hawatavumiliwa.
Mbona hii picha ya zamani sana..
Nadhani mod mnaicheki kuverify
 
Back
Top Bottom