Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima ataka Masheikh wa Uamsho waachiwe na Sheria za uhujumu uchumi zirekebishwe

Hiyo hotuba ya Gwajima bungeni inamwonyesha jinsi alivyo mnafiki. Yeye ni mbunge wa kawe, na hao masheikh wa uamsho au wa arusha hawapo kawe.Na zaidi anaingilia Mambo ya mahakama.
Kutoa maoni ni unafiki?
 
Tunashukuru sana Askofu Gwajima, endelea kutetea haki hivyo hivyo.

Sisi wananchi tunatunza kumbukumbu sana juu ya watu wanaotetea haki, maendeleo na ustawi wa watu

Big up sana Askofu, Mchango wako umekaa vizuri sana!, Endelea hivyohivyo!
 
Maoni yangu. Masheikh wapo misikitini waliopo huko wasubiri tu haki za binadamu wapeleke huko Msumbiji.
 
Angalau huyu kabebwa kuingia mjengoni lakini analeta unafiki wenye manufaa kwa wengine kuliko Babu wa ilala anataka tipishwe kodi kwenye mitandao ya simu jamani da!!!

Badala ya kuunganisha nguvu ya pamoja kuwaokoa walionewa na sheria kandamizi za serikali ya JPM

Halafu eti amefunga na sasa hivi amemaliza kufuturu anesema "Alhamdulillah" wakati waislamu wenzie wanaozea ndani wanakuja kutetewa na Askofu ama kweli Dunia Hadaa Walimwengu Shujaa wewe Iddi Hassan Zungu weweeeeeee!!! ALLAH anakuona ujue
 
Ghafla kila mbunge anaanza kuongea ukweli. Mara Gambo, Mara Gwajima. Lakin alipokuwepo Magu hakuna aliekuwa anaongea ukweli
 
Kwahiyo hao masheikh wenyewe ndio walikuwa wanawamwagia watu tindikali au kwamba kuna watu wengine ambao ndio walikuwa wakimwagia watu tindikali kwa sababu za ya mahubiri ya hao masheikh?
 
AmeHAMUKA
 
Fact!
 
Gwajima mara hii kasha sahau viongozi wenzake (wakristo) waliokuwa wakipigwa risasi, makanisa kuchomwa na kutupiwa mabomu Zanzibar, Arusha, Dar, Kagera, nakadhalika

Tulia Kijana Dawa ikuingie
 
Serikali inaweza kulega kwenye mikakati ya kukuza uchumi, lakini serikali ikilega kwenye mikakati ya kiusalama hapatakua na nchi bali fujo.
Wale jamaa, wamewekwa mahali salama, kuepusha fujo na mauaji ya kipindi kile cha kumwagiana Tindikali. Ingekua ni USA wangepelekwa Guantanamo ambapo hakuna mtu ambaye ni raia wa kawaida angeweza kuwaona. Lakini hapa busara imetumika. Kwa yale makosa walitakiwa wawe wame....
Sio Kikwete, sio magufuli wala samia atathubu kuwatoa. Ikifika hatua hiyo basi watakua wamejipanga kwelikweli. Lakini kwa upeo wangu itakua ngumu. Nchi hii zile Tunu za taifa ndizo zinalindwa kwa damu na jasho, ukitaka kupotea basi mess up na hizo Tunu
 
Kutoa maoni ni unafiki?
Kwani haelewi kwamba bunge halipaswi kuingilia mhimili wa mahakama. Mwanasheria wa serikali yupo,mkurugenzi wa mashtaka yupo,jaji mkuu yupo. Yeye anawaona walipolinyamazia hilo swala miaka yote hiyo hawana akili. Na yeye ndio mara yake ya kwanza kuingia bungeni. Hayo maoni yake yanaonyesha jinsi asivyoelewa mipaka yake kama mbunge, kwa kuingilia mambo ya mahakama.
 
Tuliona watu wakimwagiwa tindikali bcoz of them, na walipokamatwa hali ikatulia
Unaonaje hili huenda liliratibiwa na System KuBlock Wazenj wasiidai nchi yao?
 
Anajua kujiposition kwani kwa namna yeyote ile mama lazima awaachie, ili ijulikana kama mmoja wa watetezi ila nakuhakikishia Mungu anajibu
 
Kama hali ilivyotulia baada ya Jiwe kufa au?
 
“Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake wala msizozane msije mkaharibikiwa na kupoteza nguvu zenu na vumilieni (stahimilineni) bila shaka Mwenyezi Mungu yupo pamoja na wanaovumilia.” [Qur’an, 8:46].
 
Tuliona watu wakimwagiwa tindikali bcoz of them, na walipokamatwa hali ikatulia.
Sio kweli acha UONGO mtu wewe.. Leta ushahidi kwamba walihubiri kumwagiwa watu tindikali.. Chuki haitakufikisha popote
 
Hakuna maana ya kua na sheria sasa kama wanaigopa huu ndio upuuzi wa mtu mweusi sheria ifuatwe kama ilivyo hayo mengine ni uonevu tuu. Na wanaokandamiza sherua nakudhulum Mungu awaangamize
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…