Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE EDWARD LEKAITA AKAGUA MIRADI YA MILIONI 390 KATIKA KATA YA KIPERESA, KITETO
Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita ameendelea na ziara yake katika maeneo mbalimbali ya Jimboni katika Kata ya Kiperesa na kukagua Ujenzi wa Miradi katika Sekta ya Elimu, Afya, Maji na Barabara yenye zaidi ya thamani ya shilingi milioni 390,000,000.
Mhe. Lekaita alikagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa zaidi ya shilingi Million 300,000,000 bomba la Maji na Tanki la Maji katika Shule ya Sekondari Kiperesa ambapo mradi huo unajengwa na RUWASA.
Aidha, Mhe. Edward Lekaita alifika kituo cha Afya cha Mwanya kukagua vifaa tiba vipya vilivyopelekwa katika kituo cha Afya cha Mwanya ambavyo ni Vitanda na vifaa tiba vingine na Mradi wa Barabara wenye thamani ya shilingi milioni 40,000,000
Pia, alikagua Mradi wa Barabara wenye thamani ya shilingi 40,000,000; Mradi wa Dasara 1 Shule ya Msingi Chakano unaogharimu shilingi 12,500,000; Mradi wa Vyoo Shule ya Msingi Chekanao wenye thamai ya shilingi milioni 40,000,000
Mhe. Edward Ole Lekaita alifanya Mkutano wa Hadhara akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chekanao kwaajili ya kusikiliza kero zinazowakabili huku afikika kusikiliza wananchi wa Mwitikira ili kuwasikiliza nao changamoto zao kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.