Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mbunge wa Jimbo la Lulindi, Issa Ally Mchungahela, amezitaka mamlaka zinazohusika na uteuzi wa viongozi kuhakikisha zinatoa ushauri wa kitaalamu kwa Rais, ili kuepuka changamoto zinazotokana na uteuzi wa baadhi ya viongozi serikalini.
Akizungumza Bungeni wakati wa kuchangia Hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mchungahela alisisitiza kuwa Rais ni binadamu kama wengine na anaweza kufanya maamuzi sahihi zaidi iwapo atapata ushauri wa kina na wa weledi kutoka kwa wasaidizi wake