Sasa linchi la kishua namna ile kila mtu anapenda kufika/kuishi hapo, hata maadui wake wanamezea mate maisha ya pale, hata kama ni wewe utashindwa kulipenda mkuu?
Nchi ina bata za kila aina, pesa ikitafutwa inapatikana, huduma za kijamii ni za viwango vya juu, viongozi wana akili timamu na wanawaheshimu wananchi wao hakuna kuambizana jadilini uganga wa kienyeji wala kung'ang'ania madaraka, hakuna kuambizana kuwa hata msipopiga kura chama twawala kitashinda inategemea anayehesabu na kutangaza, hakuna laana za sisiem, hakuna uchawa, hakuna kumsujudu rais ili kupata teuzi, kuwa mpinzani si sawa na uhaini, hakuna simba na yanga za kutumika kupumbaza watu, hakuna kutekana wala vita, mifumo ya nchi ipo hai na inafanya kazi sustainably nk nk, at least kila kitu kinaonesha ni binadamu wanaishi na wana ubongo.
Yaani hadi raha kutaja jina la nchi yako, hata wimbo wa taifa na bendera ya nchi yako unavionea fahari. Tanzania ili uwe mizalendo na uhesabike unaipenda nchi sharti uwe ccm na umsifu rais!