Mbunge wa Mathare alazwa hospitalini baada ya kupigwa risasi nchini Kenya

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mbunge wa Mathare, Anthony Oluoch, amelazwa hospitalini Jumapili ya leo Novemba 19 baada ya kujeruhiwa katika hali tatanishi, katika mtaa wa Baba Dogo jijini Nairobi, kwenye mkutano uliohutubiwa na kinara wa NASA Raila Odinga.

Bw. Oluoch alikimbizwa katika Hospitali ya Nairobi akiwa na jeraha la mguuni ambapo NASA ilidai alipigwa risasi na polisi, huku baadhi ya ripoti zikisema kwamba alianguka kutoka kwenye gari lake wakati wa mkutano huo.

Bw. Odinga alikuwa amefika mtaani humo, baada ya madai kwamba watu kadhaa kutoka jamii fulani walikuwa wameuawa usiku wa kuamkia jana katika hali isiyoeleweka.

Hata hivyo viongozi wa NASA walimtembelea hospitalini walidai kwamba polisi walikuwa wamelenga kumuua, kwa kumpiga risasi, ila wakashindwa.

Na ingawa wanahabari hawakuruhusiwa kumwona Mbunge huyo, Bw. Odinga alikashifu tukio hilo akisema kwamba polisi sasa wameanza kuwageukia viongozi, baada ya kuwaua wananchi.

"Hii ni dalili ya mwanzo mbaya kwa taifa letu, polisi wameanza kutumika na serikali kuwamaliza viongozi wa upinzani", alisema Raila kwenye kikao na wanahabari hospitalini hapo.

Hilo linajiri baada ya Mbunge wa Kathiani, Robert Mbui (Wiper) kujeruhiwa baada ya makabiliano makali kuzuka kati ya polisi na wafuasi wa NASA, Ijumaa, wakati Raila Odinga akirejea nchini kutoka ziara ya siku 10 barani Ulaya.
 
Sasa wanakataa kuwaruhusu wanahabari wanaficha nini? Anaweza kuwa hajapigwa ni sababu tu za failure man Odinga.
 
Siasa za Afrika huzaa mambo ya ajabu sana..!
 
Kenya ni baba wa demokrasia
Wao ni mfano bora


Tuwaigeni
 
Serikali ya Uhuru its now orienting Kenya into a fragile state.

Kenyatta is a very pathetic creature.
 
Sasa wanakataa kuwaruhusu wanahabari wanaficha nini? Anaweza kuwa hajapigwa ni sababu tu za failure man Odinga.
Yote yawezekana. Ila picha eneo la tukio lilionyesha amejeruhiwa ambapo hata kutembea alihitaji usaidizi.
 
Hakuna nchi inaifkia kenya
Kwa siasa
 
Hii imekanushwa na Odinga, jamaa hakupigwa risasi. Fuatilia account ya tweeter ya Odinga kupata ukweli kilichomsibu
 

That report has been rubbished.
Hakupigwa risasi. Alianguka na kupata fracture ya mguu.
 
Propaganda za NASA hizi walitaka apigwe risasi ndo iweje sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…