Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Bw. Oluoch alikimbizwa katika Hospitali ya Nairobi akiwa na jeraha la mguuni ambapo NASA ilidai alipigwa risasi na polisi, huku baadhi ya ripoti zikisema kwamba alianguka kutoka kwenye gari lake wakati wa mkutano huo.
Bw. Odinga alikuwa amefika mtaani humo, baada ya madai kwamba watu kadhaa kutoka jamii fulani walikuwa wameuawa usiku wa kuamkia jana katika hali isiyoeleweka.
Hata hivyo viongozi wa NASA walimtembelea hospitalini walidai kwamba polisi walikuwa wamelenga kumuua, kwa kumpiga risasi, ila wakashindwa.
Na ingawa wanahabari hawakuruhusiwa kumwona Mbunge huyo, Bw. Odinga alikashifu tukio hilo akisema kwamba polisi sasa wameanza kuwageukia viongozi, baada ya kuwaua wananchi.
"Hii ni dalili ya mwanzo mbaya kwa taifa letu, polisi wameanza kutumika na serikali kuwamaliza viongozi wa upinzani", alisema Raila kwenye kikao na wanahabari hospitalini hapo.
Hilo linajiri baada ya Mbunge wa Kathiani, Robert Mbui (Wiper) kujeruhiwa baada ya makabiliano makali kuzuka kati ya polisi na wafuasi wa NASA, Ijumaa, wakati Raila Odinga akirejea nchini kutoka ziara ya siku 10 barani Ulaya.