Mbunge wa Mbeya Mjini, Patric Mwalunenge, Juni 20, 2026 ameingia kwenye kadhia ya kuzomewa na Bodaboda pamoja na machinga kwa kuwataka wachangie kiasi cha shilingi 1,000 kila mmoja kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Mwalunenge amekumbana na zomeazomea hiyo wakati wa kikao chake cha majumuisho na makundi hayo jijini Mbeya, ambapo alijaribu kufafanua mchango wa sekta isiyo rasmi kiuchumi, akidai kuwa kipato wanachokiingiza kwa siku kinatosha kuwafanya washiriki maendeleo badala ya kujiona maskini, hoja iliyoamsha hisia kali na malalamiko kutoka kwa madereva hao.
Anachozungumza kwenye video kwa maneno
"Hapa Tunaongea mambo ya msingi kwa ajili ya maisha yenu ya baadaye...
"Nimempigia... nimempigia kiongozi wenu hapa, mmesema mnamtaka kiongozi wenu? Nimempigia simu, anasema yuko Oyole anaenda msibani, alikuwa hana habari ya hichi kikao." (Wananchi wanaanza kupiga kelele na kuzomea).
"Sasa... sasa mbona yeye ndio maana anasema... Hello? Bodaboda hoyee! Ndio maana anasema mpigieni simu nyinyi au mfuateni."
Bodaboda hoyee! Sasa wale wanaotaka kusikiliza, wale wanaotaka kusikiliza habari... wanaotaka kusikiliza basi wabaki, wanaotaka kusikiliza basi watoke. Wanaotaka kusikiliza kaeni mtulie. Msikilize, wale wanaotaka kuzungumza mimi ni nini kwa ajili ya bodaboda, kwa ajili ya maisha yenu."
"Sawa? Wale wanaotaka kusikiliza kaeni mnisikilize ninachotaka kuzungumza mimi. Ndio! Ndio! Kwa hiyo mnaotaka kusikiliza kaeni hapo ili msikilize ninachotaka kusema, wale ambao hawataki kusikiliza waache waondoke. Kaa chini mtulie msikilize."
"Bodaboda hoyee! Kaeni chini basi mshike adabu mnisikilize mimi. Sawa? Wale wanaotaka kuondoka waondoke, wanaotaka kusikiliza wasikilize. Sawa? Haya nasubiri mkae mtulie tuwasikilize."
"Mnaotaka kusikiliza msisikilize... mkiwemo Chapa Chapa, mkikaa mkaamua hivo Chapa Chapa mnaelewa mnaonyesha nini. Itakuwa mende mkafanye kazi zenu. Sawa bwana? Bodaboda hoyee!"
Wala mimi niwaambie, kwenye haya maisha tuna mambo haya mawili unaweza ukachagua. Unaweza ukaamua wewe mwenyewe upate shida au upate raha kulingana na tabia yako. Wewe kama unaweza ukaingiza shilingi elfu kumi au elfu ishirini kwa siku, unataka ajira ya nini? Unataka ajira ya nini?"
"Cha msingi sisi ni kukuwezesha ukae vizuri, uheshimike, usibughudhiwe kwenye kazi zako, usisumbuliwe. Mpe mafunzo, mwendeshe leseni... hawa hapa VETA wako hapa. Mimi nimeshatoa milioni 16 kule Kwimba kwa ajili ya kuwafundisha wale bodaboda kupitia VETA, mimi nimetoka kwenye mkoa wa dar es salaam washaanza kuitumia...".
"Nawaombeeni sana... mji umejibu. Sasa hivi pale Kwimba, wale bodaboda na makundi mbalimbali, nadhani Jumanne au Jumatano wanapewa cheki ya milioni 340. Ziko wapi hapa 340? Kupitia programu hii ya mbinu, vijana wa bajaji, bodaboda na wale wanaouza mboga mboga, milioni 300 wanapewa... 340 cheki."
Pia soma: Taifa la Fremu, Boda na Bajaji , Je, Hii ndiyo Ndoto ya Kijana wa Kitanzania?