Ikiwa ni msimu wa sita kwa Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Akson kugawa bima na mahitaji muhimu kwa kaya 1500 sawa na wazee 9000 wa Jiji la Mbeya, Dr Tulia amewataka wenyeviti wa mitaa ya Halmashauri ya Mbeya kuendelea kuwaibua wenye uhitaji ili wasaidiwe na taasisi hiyo pamoja na wadau mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zubeir Homera amemshukuru Mkurugenzi wa Tulia Trust Dkt Tulia Ackson kwa kuziunganisha wilaya zote za Mkoa wa Mbeya kwa kuwapatia misaada kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwajengea nyumba watu wenye mahitaji maalumu.
Hata hivyo baadhi ya viongozi akiwemo Chifu wa Mkoa wa Mbeya Rocket Mwashinga na Naibu Meya wa Jiji la Mbeya Kefas Mwasote wameeleza namna Dkt Tulia anavyowapambania na kuwathamini wakazi wa Mbeya.
Nadhani kati ya wabunge wenye hali ngumu jimboni ni huyu Mmama. Anajua fika Sugu alipata umaarufu kabla yake.. Na alianza harakati akifanya mziki kama kazi. Halafu pia jinsi ina msumbua anaona wazi kupambana na kidume ujipange.. Ashukuru ni spika.. Unless ataangukia pua..

Je! Kama siyo rushwa ni nini?
Je! Ni zawadi ama?
Je! Pesa ni yake binafsi ?
Je! Pesa ya ofisi ya bunge?
Je!pesa ya ofisi ya mbunge?
Je! Pesa hizo ni za umma?