Mbunge wa Mlimba, Godwin Kunambi: Tujenge 'Monument' ya kumuenzi Hayati Dkt. Magufuli jijini Dodoma

Mbunge wa Mlimba, Godwin Kunambi: Tujenge 'Monument' ya kumuenzi Hayati Dkt. Magufuli jijini Dodoma

Kazi zake na matokeo ya hizo kazi! Ndo inamfanya aseme hivyo. Sasa kikwete ajengewe ndege inayoenda angani na kusema rais wa angani au?? JPM amepiga kazi ndugu! Kama alikutumbua! Pole kwa hilo. Na hauna haja ya kulaumu! ni vyema ukaangalia ni wapi ulikosea.
Kazi ipi alifanya Magufuli? Kupora uchaguzi wa mitaa na uchaguzi mkuu?
 
Ule uwanja wa Ndege Porini si kumbukumbu tosha

Hakuna haja ya Sanamu
 
Vipi kuhusu muasisiwa wazo la kuhamishia makao makuu Dodoma, Hayati Mwl Nyerere?

Kuhamia Dodoma kumehusisha masuala mengi ambayo serikali zote zilizopita zimefanya,na hivyo kumekuwa na muendelezo yangu serikali ya Nyerere.

Awamu iliyopita,kwa mfano,pamoja na mambo mengine walijenga ukumbi wa kisasa wa bunge. Kumbuka ,zamani vikao vya bunge vilifanyika Dar.

Kama ni monument,anayestahili ni Nyerere. Basi. Hakuna mwingine.
 
Huyu dogo yaan kwa kua jiwe alimpa ubunge Kama zawadi kwa kupora haki ya wananchi kuchagua kwa kuwaengua wagombea wengine ndo anataka atushirikishe wote hio laana ya wizi.
 
Kazi zake na matokeo ya hizo kazi! Ndo inamfanya aseme hivyo. Sasa kikwete ajengewe ndege inayoenda angani na kusema rais wa angani au?? JPM amepiga kazi ndugu! Kama alikutumbua! Pole kwa hilo. Na hauna haja ya kulaumu! ni vyema ukaangalia ni wapi ulikosea.
Kila awamu imefanya mambo makubwa!

Tatizo lenu wapambe mnataka kudanganya umma kwamba Magufuli tu ndie kafanya.

Kwa mfano mmoja tu, chuo kikuu cha Dodoma alijenga nani?

Acheni wivu bana!
 
Wabunge wa jiwe waliopita bila kupingwa kwa fadhila ya jiwe.
 
Hili jimbo wabunge wake wanapenda sana masanamu sijui kwa nini?
Yule aliepita nae alikuwa anataka ijengwe sanam ya Diamond!
Ndugu zangu wa Mlimba mnafeli wapi ?
 
Kwa kitu gani cha maana alichotuachia zaidi ya wizi wa fedha za umma, chuki, ubaguzi wa kikabila na kikanda, utekaji na uuaji?

Kimambi ana sura Kama kijana lakini akili ya kizee. Kwa hiyo watu wa Mlimba ndiyo wamemtuma huo UJINGA?
 
wabunge wengi walishindishwa ubunge na JPM sasa jamaa ndo hivyo hayupo tena hapo wanasikitika 2025 mambo yatakuwa magumu
 
...hiyo sanamu akaijenge nyumbani kwake kama ame mmisi sana mwendazake
 
Marais wakristu ni wabinafsi sana. Mbona hamna mtu anasema tujenge sanamu ya Kikwete. Hivi hawa watu wamelogwa au ni nini? Huyo magufuli mpora uchaguzi ndiyo wanamwona wa maana
Mjenge sanamu ya kikwete ili kuenzi ufisadi au kushamiri kwa biashara ya madawa ya kulevya? Anayesema ijengwe ni rais mwenyewe au mtu baki kutokana na kile anachofikiria yeye? Usiendekeze udini mtanzania wewe maskini na mwenye umri mdogo.sisi tuliokuwepo toka miaka ya uhuru tunafaham mengi ukiacha wewe dogo wa miaka hii ya tisini mwishoni.
 
Kazi zake na matokeo ya hizo kazi! Ndo inamfanya aseme hivyo. Sasa kikwete ajengewe ndege inayoenda angani na kusema rais wa angani au?? JPM amepiga kazi ndugu! Kama alikutumbua! Pole kwa hilo. Na hauna haja ya kulaumu! ni vyema ukaangalia ni wapi ulikosea.
Na nyinyi ndio mliomponza,akajiona Muungu. Kuua,kuteka,bidhaa bei juu,na ufisadi uliofuchwa,
Huyu hata kwenye vitabu asiwekwe.

🏌️🤦
 
Anza na nyerer baba wa taifa alafu mkapa then maalim seif afu yeye unaemtaka kama ndio hivo
 
Kunambi huo upambe auache. Tuna changamoto sana wana Mlimba za kutusemea huko Dodoma. Sasa anasimama kutetea sanamu kujengwa kitu ambacho hakimsaidii mwananchi wa Mlimba kuboresha maisha. Kunambi jitizame na kujifanyia tathmini juu ya upeo wako. Acha kusema hovyo kwa mihemko yako binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom