Pre GE2025 Mbunge wa Ngara na Diwani Wamlilia Rais Samia kujenga barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 114 kutoka Murugarama Rulenge

Pre GE2025 Mbunge wa Ngara na Diwani Wamlilia Rais Samia kujenga barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 114 kutoka Murugarama Rulenge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Katika mkutano wa hadhara wa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohammed Kawaida, Mbunge wa Jimbo la Ngara Ndaisaba Ruholo ameomba serikali kujenga barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 114 kutoka Murugarama Rulenge.

Mbunge huyo amesema kuwa kila walipokuja kuomba kura kwa wananchi wamekuwa wakiahidi ujenzi wa barabara hiyo suala ambalo limekuwa halitekelezeki na kuondoa imaani kwa wananchi.

Amemuomba Kawaida kumfikishia maombi ya wananchi wa Ngara kuhusu barabara hiyo ambayo ipo kwenye bajeti ya nchi lakini fedha za utekelezaji wake haufanikiwi.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Bugarama Theofilda Lwota amesema kutokana na kukua kwa kata hiyo ambayo ina shule moja ya sekondari kujengewa bweni ili kuweza kuwanusuru watoto wanaotembea umbali mrefu.

Aidha diwani huyo ameendelea kuomba kuwa kata hiyo kubwa inachangamoto kubwa ya kituo cha afya ambao ameeleza wananchi wake wanatembea umbali mrefu kutafuta huduma ya afya.

Sambamba na hilo diwani huyo ameomba wananchi wake kulipwa fidia ya kupisha mradi wa barabara ambayo wameisubiri kwa kipindi cha Zaidi ya miaka mitatu bila mafanikio.
 
Back
Top Bottom