Mpepetaji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 346
- 213
Serikali imeshauriwa kuweka bei elekezi ya uunganishaji wa umeme maeneo yote nchini ili kuwawezesha wananchi wa mijini na vijijini waweze kupata huduma hiyo.
Ushauri huo umetolewa leo Jumatatu Aprili 28,2025 bungeni Jijini Dodoma na Mbunge wa jimbo la Nyang'hwale Hussein Nassor wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Amesema “leo hii serikali imeamua kumfungia mwananchi kijijini umeme kwa gharama ya shilingi elfu 27 lakini kuna wananchi ambao wako mjini na maisha yao na nyumba zao nikama zile za watu wa kijijini kwanini na hawa wananchi walioko mjini wasifungiwe kwa shilingi elfu 27 tuondokane na ile shilingi laki 5 ama zaidi ya laki tano,”