Akizungumza na wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Kata 3 za Nyamagaro kyang'asaro na Nyamtinga, Mbunge wa Jimbo la Rorya, Jafari Chege amewawetaka wananchi wa Kata hizo kutambua dira ya maendeleo tangu walipokuwa, walipo sasa na wanakoelekea.
Chege ameendelea kuwapa ushirikiano wananchi wa Rorya na kuwaahidi makubwa kwani bado ana uwezo wa kuwahudumia na kuwatumikia wakazi wa jimbo lake kwani maendeleo ndio kipaumbele chake.
"Tunatambua umuhimu wa maendeleo na miradi mingi ya kimakakati inayoletwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili yetu sisi wana Rorya hivyo tunapaswa kushukuru kwa kila hatua tunayopiga kwenda mbele kimaendeleo" Amesema Mbunge Chege