Poleni sana familia ya Marehemu Ng'itu. Mungu amlipe kwa mema aliyoyafanya na awape subira wale wapendwa wake aliowaacha, kwani sote tutaishia huko.
Wakati huu wa kifo, hasa cha mtu unayemfahamu, ndio wakati wa kujikumbusha kuwa hapa duniani tuko transit tu na huwezi kujua wapi na nani atakuzika.
Kwa hiyo ndugu zangu tumche Mungu, tupendane, tusaidiane na tushirikiane. Tauche magomvi, fitna, husda, ufisadi na wivu kwani muda wetu wa kukaa hapa duniani ni mfupi sana ukilinganisha na huko Ahera ambapo malipo meme utayapata kwa mambo yaliyokuwa marked na BLUE wakati yale yaliyo katika RED ni balaa tupu ndizo utazozipata.. Amen