Uchaguzi 2020 Mbunge wa Same Magharibi, Dkt. Mathayo David ahojiwa na TAKUKURU

Uchaguzi 2020 Mbunge wa Same Magharibi, Dkt. Mathayo David ahojiwa na TAKUKURU

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
53378F5F-97C0-4950-9AA7-2294F08B4574.jpeg

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inayashikilia magari 10 ya wagonjwa ambayo yalikuwa yagawanywe kwa kata 10 za Jimbo la Same Magharibi na Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Mathayo David kama utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa mwaka 2015.

Magari hayo yalikuwa yagawanywe kwa kata hizo jana tarehe 08.07.2020 kupitia ofisi za CCM Wilaya ya Same lakini TAKUKURU ikaingilia kati na ikamuita Dkt. Mathayo na kumhoji kuhusu tukio hilo, kuelekea mchakato wa kupata wagombea ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu
 
Bila rushwa hakuna ccm
Yaani CCM bila rushwa huwezi fika popote!! Na ni wote tu, hakuna asiyetoa rushwa!! Watu wa namna hiyo waje wawe na uchungu na mwanachi?!! Wewe subilia baada ya kura za maoni kupigwa, utawaona watakavyo ruka na kukanyagana!!!

Kama wale walio hamia huko ndio nawahurumia kabisa!!! Labda rungu la mwenyekiti la kutoangalia aliyeongoza kwenye kura za maoni litumike!!!
 
Ninashauri atimize ahadi yake ya kuwapatia magari ya wagonjwa.akisha maliza ccm ikate jina lake na Jimbo lipewe mwanachama kwingine.hii ni rushwa ya mchana peupeeee. Bado Shaly Raymond atolewe pia kwenye viti maalum.
 
Wamuache atoe magari kina mnyika hata baiskeri hawawezi kugawa kwa miaka 20
Na upinzani ndio ulifanya hata vijana ambao hawakuwa na pesa kuingia bungeni!!enzi zile kabla Demokrasia haijanajisiwa!! Kitu ambacho kwa ccm ni ngumu, ccm kama hutoki familia ya wateule, na huna pesa kushinda ubunge ni ndotooo!!
 
View attachment 1502131

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inayashikilia magari 10 ya wagonjwa ambayo yalikuwa yagawanywe kwa kata 10 za Jimbo la Same Magharibi na Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Mathayo David kama utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa mwaka 2015.

Magari hayo yalikuwa yagawanywe kwa kata hizo jana tarehe 08.07.2020 kupitia ofisi za CCM Wilaya ya Same lakini TAKUKURU ikaingilia kati na ikamuita Dkt. Mathayo na kumhoji kuhusu tukio hilo, kuelekea mchakato wa kupata wagombea ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu
Huyu anawajali wapiga kura wake kuliko yule aliyewanunulia baskelii kule Nzega au gari la kuzikia kule ugogoni!
 
Akili za kuku utazujua tu mnyika anaingiaje kwenye issue ya Same sijawahi kuona ukiandika cha maana humu
Huwezi kuona maana akili zako kama za mbowe kichwa kimejaa matope tu
 
Watanzania sijui nani katu loga. Yaani miaka mitano leo ndio ana leta hongo?
Alikuwa wapi muda wote huo? Wenzake waligawa mwaka wa kwanza na mengine tyari yako juu ya mawe.
 
Yaani alishindwa kuwaletea Wana Same magari hayo kwa kipindi chote alichokuwa Mbunge, Leo ndo anawakumbuka? Hii kweli Rushwa. Nashaur magar hayo yagawiwe kwa wananchi Kisha Chama wamkate, ili iwe funzo kwa wote wenye tabia hizo.
 
huu ubunge una faida gani haswa hadi unatafutwa kwa udi na uvumba !?!?!?
 
Mbaya kugawa kanga na fedha taslimu
Lakini magari ya wagonjwa?!kwa hiyo hawataki zahanati ziwe na ambulance?
 
Bila rushwa hakuna CCM
Rushwa huko kwenu, kwa Magari ya wagonjwa hapa kwetu ni msaada wa lazima kwa Jamii, hasa wakazi wa milimani kama Vudee, Mbaga, Mvaa, Kisiwani,Gonja na hata jImbo la Mwanga maeneo kama Jipe, Kifula, Kighale, Kileo, Kilomeni, Kirongwa, Kirya, Kwakao, Lang'ata, Lembeni, Msangeni, Mwaniko, Ngujini na Shingatini leteni hizo Ambulance tena haraka. kama na wengine wapo nani kawazuia walete tuu hata kugawa ng'ombe, mbuzi ada za wanafunzi wa secondari za A level.

Wakiwa bungeni wanakula wao, sasa ni muda muaafaka na sisi wapiga kura tupate chambi chambi. Go Matayo gooooooooo.
 
Back
Top Bottom