Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, amewahimiza wakazi wa jimbo lake kumpigia kura Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Akiwa katika ziara yake, Katambi alikutana na Wajumbe wa CCM wa Kata ya Kizumbi na Ibinzamata, kisha kufanya mkutano wa hadhara. Amesema ndani ya miaka minne ya ubunge wake, ameleta maendeleo makubwa Shinyanga na kutekeleza ahadi zake, akimshukuru Rais Samia kwa kumuunga mkono.
Ametaja miradi ambayo ameitekeleza kila sekta, upande wa elimu kipindi anaingia kwenye ubunge Shinyanga Mjini, kulikuwa na shule 65 za Msingi na sekondari, lakini wamejenga shule mpya 10 mpya.
Akisema hadid sasa wamefikisha shule 75, pamoja na kujengwa pia shule ya wasichana, ambayo haikuwapo, huku wakitatua pia tatizo la upungufu wa walimu kutoka 421 hadi 180.
Amesema pia wanapanua Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Kizumbi, zimepatikana kiasi cha fedha Sh. bilioni 11 kwa ajili ya kuongeza majengo, ili kiwe na wanafunzi 3,000 pamoja na kuwapo na mikakati ya kupanua Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto na pia wameleta Tawi la Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, kuongeza mzunguko wa fedha.
“Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ni Mwadilifu, Mmwaminifu, mzalendo anayetekeleza, hivyo naombe mpigieni kura nyingi za ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu 2025, sababu Shinyanga Mjini, ameitendea haki, ndani ya miaka minne ya ubunge wangu imepiga hatua kubwa na bado anazidi kumwaga pesa,”
“Kazi ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo kichwani mwanamke ipo pale pale, ndiyo maana anatoa fedha na miradi mingi ya maji inazidi kutekelezwa, Mama ukimuomba anasikia na kutekeleza,”
Source: Nipashe