Biashara inaendele!!
Wahame tu ila wananchi tuko na CHADEMA/upinzani maaana CCM na Magufuli hawana msaada kwetu.Pia sidhani kama upinzani kuna mapungufu yanayoweza kuhalalisha hamahama hii katika mazingira haya yenye utata hasa ukitazama na mapungufu ya hii serikali wanayodai kuinga mkono.
Maisha ya mtanzania sio ndege, flyover, Chato Airport, banadari ya Chato, n.k, bali ni pamoja na bei nzuri ya mazao ya wakulima, ajira, mishahara na masilahi bora kwa watumishi, uhuru wa maoni, mikopo elimu ya juu bila ubaguzi, elimu bora ni si bora elimu, kodi rafiki kwa wafanyabiashara, n.k.
Maisha ya mtanzania ni watoto kutokusoma shule za nyasi na kukaa kwenye vumbi, watanzania kuto-share maji na mifugo,bei za bidhaa kutopanda, watanzania kutopoteza ajira kwasababu biashara zinakufa na makampuni kufungwa au kuyumba, n.k.
Ni watawala hawa, bila kujali kuwa vipato vya watanzania viko chini ikiwemo mishara duni,wamenongeza makato ya Bodi ya mikopo karibu mara mbili huku wakisema serikali hii ni ya wanyonge! Alafu wewe mbunge unaepaswa kuwa mtetezi wa wananchi, unaunga mkono serikali ya aina hiyo!!Unajua wajibu wako wewe kama mbunge kweli!!Pathetic!
Ni katika awmu hii pia tumeshuhudia bomoabomoa ya hali ya juu huku wananchi wakitseka licha ya baadhi yao kudai walikuwa na zuio la mahakama nyumba zao zisibomolewa ila wahusika hawakujali na mpaka tukasikia Benki ya dunia ikatishia kutotoa fedha kwasababu ya hiyo bomoabomoa alafu wewe mbunge hujiuliza tu kuhusu haya!
Kuna watu mpaka leo hawajulikana walipo huku serikali ikiwa haina majibu, alafu wewe mbunge, tena wa upinzani, unaunga mkono serikali ambayo mpaka leo imeshindwa kutoa majibu ni wapi watanzania wenzetu hawa walipo kisa sijui serikali imenunua ndege na mambo mengine ya aina hiyo!!!!Haingi akili hata kidogo!
Serikali hii mpaka sasa imeshindwa kutekeleza baadhi ya ahadi zake ikiwemo kutoa milioni 50 kwa kila kijiji, alafu wewe mbunge, tena wa kutoka kambi ya upinzani, badala ya kuitaka serikali itimize ahadi yake, ndio unaenda kuunga mkono juhudi za aina hii!!Inasikitisha!
Pia,watanzania hatutaki mtu asietaka kukosolewa, anaetuletea sheria za kutuziba midomo mfano sheria ya takwimu, kiongozi asiethamini demokrasia na asieheshimu maamuzi ya wapiga kura.kiongozi anaevunja katiba na sheria za nchi tena wazi wazi.
Watanzania hatuhitaji mtu asie na kauli za staha ambae anaweza kuongeoa lolote na mahali popote.
Waendelee kuwalipia madeni na mikopo kama inavyodaiwa na wabunge wenzeo ila wasitake kutuhadaa kisa matumbo yao.
Never ever hatutadanganyika na haya maigizo yenu na huyo mnaemsujudia.
Kibaya zaidi hakuna mnacho-achieve, sana sana mnazidi kuiogopa CHADEMA na kuona sanduku la kura kama mtihani uliowashinda katika maisha yenu!
CCM hii ni ndoto kubadili maisha ya watanzania kwani miundombinu pekee sio muarobaini wa kuleta japo unafuu kwa maisha ya mtanzania.
Hakuna nchi ilioendelea kwa wabunge au madiwani kujiuzulu na kumuunga mkono Raisi alie madarakani na kusababisha nchi kuingia gharama kubwa za marudio ya uchaguzi kila kukicha.Hakuna!
Mnatutia aibu watanzania!
Poor you!
Nyinyi ndio wale Mwalimu aliwaita mercenaries!