Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Sumve (CCM), Kasalali Mageni leo Jumanne Mei 6, 2025 amekuwa mbunge wa kwanza kusikika akipinga bajeti ya Serikali kwa madai ya kuchoshwa na uongo.
Mageni ameipinga bajeti ya Wizara ya Ujenzi iliyowasilishwa jana Jumatatu, Mei 5, 2025 na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ambaye aliomba Bunge limpitishie Sh2.28 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi mengine.
Kauli ya Mageni inakuwa ya kwanza kusikika tangu mkutano wa 19 katika Bunge la 12 maalumu la kujadili bajeti za Serikali jijini Dodoma tangu ulipoanza Aprili 8, 2025 ambapo wabunge wamekuwa wakiunga mkono tangu kuanzia hotuba ya Waziri Mkuu na zilizofuata.
Amewataja marais watatu, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, John Magufuli ambao kwa nyakati tofauti walipofika wilayani humo, Mkoa wa Mwanza waliahidi ujenzi wa barabara lakini hilo halikufanyika na wilaya hiyo imeendelea kutounganishwa kwa lami.
Akijibu hoja hiyo, Waziri Ulega amesema: "Mtani wangu usiwe na wasiwasi, nimekusikia na jambo lipo katika vitabu. Nataka nikuhakikishe nina safari ya Mwanza, nitakwenda hadi Sumve na ninajua sasa hivi watani mnapenda sana maendeleo na mimi nataka usikasirike na hutaharibikiwa kwa sababu ya barabara."