DodomaTZ
Member
- May 20, 2022
- 84
- 118
Mbunge wa Sumve, Kasalali Mageni amechangia Bungeni Jijini Dodoma, leo April 4,2024 ambapo katika mchango wake amemuomba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kuzungumza na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kutekeleza majukumu yao ya kuwezesha suala la maendeleo ya kujengwa Barabara ya lami katika jimbo lake Sumve.
Kasalali amesema kuwa Wananchi wa jimbo lake wanachotaka kwa sasa ni suala la barabara ya lami na sio jambo lingine.
Kasalali amesema ameshajaribu kuzungumza na mawaziri hao lakini bado wamekuwa wakimpa maneno mengi bila kuwa na utekelezaji jambo hilo.