G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Kwa mujibu wa mbunge Godbles Lema na Waziri Kigwangalla ni kuwa mbunge wa Sumve Richard Ndassa amefariki dunia mapema leo.
Aidha taarifa zinasema kuwa Ndassa amefikwa na umauti baada ya kuanguka ghafla ndani ya viwanja vya bunge leo.
Inadaiwa pia kuwa ndani ya hoteli aliyokuwa akiishi kumepatikana vifaa vya kujifukiza.
Mchango wa Ndassa bungeni kuhusiana na Ugonjwa wa Corona:
BUNGE LAAHIRISHWA
Spika wa Bunge, Job Ndugai, leo Aprili, 29, 2020, ameahirisha Mkutano wa 19, Kikao cha 9, cha Bunge hadi kesho, kufuatia kifo cha Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa.
Ndassa anakuwa mbunge wa pili wa CCM, kufariki dunia wakati Mkutano huu wa Bunge la 19 ukiendelea, baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mchungaji Getrude Rwakatare kufariki dunia wiki iliyopita.
“Waheshimiwa wabunge, ninaomba kuwajulisha kuwa bunge letu limepata na msiba mwingine mkubwa wa kuondokewa na mbunge mwenzetu wa Jimbo la Sumve ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo hapa Dodoma.
“Kufuatia msiba huo, taratibu mbalimbali za mazishi zimeanza kufanyika kwa mawasiliano kati ya Ofisi ya Bunge na familia ya marehemu na serikali na kila tukipata taarifa zadi za kuwataarifu tutafanya hivyo,” amesema.
Aidha, akimueleze Ndassa, Spika Ndugai amese; “Marehemu Ndassa ni mmoja wa wabunge waliokuwa wanaitwa senetors, alikuwa ni mmoja wa wabunge waandamizi walioingia bungeni tangu mwaka 1995, amekuwa mbunge wa Sumve kwa vipindi vitano na miezi… hii inaonyesha imani kubwa waliyokuwa nayo wananchi wa Sumve na wabunge wengi tunaweza tukajifunza uongozi bora kwa kufuata nyayo zake.
Pamoja na mambo mengine, Spika Ndugai amesema kwa mujibu wa Kanuni ya 151 ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la 2016, kwa siku ya leo hawataendelea na kikao cha bunge badala yake watakuwa na maombolezo ya msiba wa mbunge huyo.
“Tutajitahidi sana iwezekanavyo kuhakikisha kwamba ndugu yetu anazikwa kule Sumve kesho jioni, tutajitahidi sana sana… kwa sababu kwa mila zetu za Kiafrika kwa kweli kumzika mtu popote pale ni jambo linalotupa ugumu fikiria wote tuliopo hapa upate jambo kama hilo halafu unawekwa popote, kwa hiyo tutajitahidi sana. Kwa hiyo ofisi yangu itashirikiana na serikali kuona kila kinachowezekana kinafanyika,” amesema Spika Ndugai.
Richard Mganga Ndassa amezaliwa tarehe 21 Machi 1959 na amefariki Tarehe 29 April 2020
====
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugaina wananchi wa jimbo la Sumve Mkoani Mwanza kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Richard Mganga Ndassa.
“Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha ghafla cha Mhe. Ndassa nakumbuka mimi na yeye tulianza pamoja Ubunge mwaka 1995, Yeye akiwa Mbunge wa Jimbo la Sumve na mimi nikiwa Mbunge wa Jimbo la Biharamlo Mashariki ambalo sasa hivi linaitwa Jimbo la Chato,Namuoma Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi amina”
SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA CHAMA CHAKE (CCM)
| GENERAL | ||
|---|---|---|
| Salutation | Honourable | Member picture |
| First Name: | Richard | |
| Middle Name: | Mganga | |
| Last Name: | Ndassa | |
| Member Type: | Constituency Member | |
| Constituent: | Sumve | |
| Political Party: | CCM | |
| Office Location: | P.O. Box 88, Kwimba, Mwanza | |
| Office Phone: | +255 752 333444/+255 787 535338 | |
| Ext.: | ||
| Office Fax: | ||
| Office E-mail: | rndasa@parliament.go.tz | |
| Member Status: | Current Member | |
| Date of Birth | 21 March 1959 |
| School Name/Location | Course/Degree/Award | Start Date | End Date | Level |
|---|---|---|---|---|
| EDUCATION | ||||
| College of Business Education-CBE | Diploma in Accountancy | 1987 | 1989 | DIPLOMA |
| Tanzania School of Journalism-Dar es Salaam | Certificate in Journalism | 1985 | 1986 | CERTIFICATE |
| Buluba Secondary School | O-Level Education | 1977 | 1980 | SECONDARY |
| Company Name | Position | From | To |
|---|---|---|---|
| EMPLOYMENT HISTORY | |||
| Mfanyakazi Newspaper | Sales Manager | 1982 | 1995 |
| CCM - Chama Cha Mapinduzi | Member of Parliament of Tanzania | 1995 | 2020 |
UPDATE
SPIKA NDUGAI: Bunge litajitahidi Ndassa azikwe kijijini kwake kwa mujibu wa mila na desturi
Spika wa bunge la JMT mh Ndugai amesema watafanya kila njia kuhakikisha rip mbunge wa Sumve marehemu Ndassa anazikwa kijijini kwao kwa mujibu wa mila na desturi za jamii yao.
Ndugai amesema ofisi yake inashirikiana kwa karibu na familia ya marehemu na kwamba bunge litashiriki kikamilifu katika msiba wa senetor huyu ambaye aliingia bungeni mwaka 1995 na hajawahi kushindwa uchaguzi.