Mbunge wa Tanga, Kassim: Kwanini SGR inasema “no seat available” halafu kwenye treni zipo wazi?

Mbunge wa Tanga, Kassim: Kwanini SGR inasema “no seat available” halafu kwenye treni zipo wazi?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Tanga, Kassim Amari Mbaraka amehoji kuhusu kutopatikana kwa tiketi za Treni ya SGR kwa kuonesha kuwa No Seat Available ilihali ukiingia ndani ya Treni kunakuwa na Siti nyingi ambazo hubaki wazi.

Ametoa hoja hiyo leo Oktoba 27, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali Wizara ya Uchukuzi.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amejibu na kutoa ufafanuzi huku akikaribisha maoni ya Watanzania katika kuboresha mifumo ya SGR.


'"Mara nyingi unapoingia kwenye mfumo unakuta kwamba imeandikwa 'no seat' maana yake tumeshauza, na hii inategemeana na mambo mbalimbali. Moja ni siku; ukienda kipindi cha wikiendi kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, Watanzania wengi sana wanajitokeza kununua tiketi."

"Abiria waliosafiri ukilinganisha na waliokata tiketi ni 92%. Ambao hawakusafiri pamoja na kwamba walikata tiketi walikuwa ni abiria 781,516, sawa na 8% hawakusafiri."

"Ukichukua mwezi uliopita tu wa Septemba, tuliuza tiketi 341,214, waliosafiri walikuwa 305,871 (sawa na 90%), na ambao hawakusafiri ni 35,343 (sawa na 10%)."

Soma pia: Ushauri kwa SGR kuhusu mfumo wa ukataji tiketi kuonesha seat kujaa
 
Huyu ni waziri au ujinga..swali dogo km hilo maelezo hayaeleweki kabisa, si ya kujibu swali..jibu swali kwanza ndio ulete hizo cosmetics.
 
Kwani yeye hajui CCM wenzake wanamiliki mabasi ya Moro-dsm-Dom

Watapata wapi abiria Treni ikijaza 🙌🥲
 
Shabiby & Abood wanasemaje?
Hili swali,walishaambiana,kuwa ataliuliza,ili kuridhisha wajinga
 
Huyu ni waziri au ujinga..swali dogo km hilo maelezo hayaeleweki kabisa, si ya kujibu swali..jibu swali kwanza ndio ulete hizo cosmetics.

Mkuu mbona ameeleweka, kuna watu wanakata ticket lakini kwasababu moja au nyingine hawasafiri, mimi pia imeshawahi kunitokea. Takwimu ameweka kuonesha uhalisia wa tatizo. Nadhani wangeongeza muda wa kuahirisha safari kwasababu wateja wapo hata kwa gharama kidogo kwa mkataji wa awali.
 
Mbona hii inatokea kwa mashirika ya umma zaidi
nenda kata ticket precision air ikisema imejaa; ukisafiri unakuta imejaa kweli...
Nenda flight link/ Safari link/ Auric Air, Airlink nk ukikata ticket ukaambiwa imejaa, ukisafiri unakuta imejaa. Sasa nenda Air tanzania Unaweza kukuta imejaa; ukienda kusafiri ina 65% kwa treni nilikuwa sijafuatilia ila inaonekana kama hali ni hiyo hiyo

Swali ni je?
kwa nini mashirika ya private au ya kimataifa yanayotumia hiyo mifumo yanajaa?
AU basi niseme wanatakiwa wafanye utafiti kwa nini hiyo hali inatokea na sio kutoa tu majibu ya kimazoea..ULIMWENGU UMEBADILIKA ...UNATAKA SOLUTION NA SIO MAJIBU AMBAYO KILA MTU ANAWEZA KUYATOA....LAKINI PIA KUACHA ABIRIA SIO SIFA. Pengine waongeze option ya release seat any time within 24hrs before travel (ili ziuzike tena)
 
Mbona hii inatokea kwa mashirika ya umma zaidi
nenda kata ticket precision air ikisema imejaa; ukisafiri unakuta imejaa kweli...
Nenda flight link/ Safari link/ Auric nk ile inaenda Nairobi, ukikata ticket ukaambiwa imejaa, ukisafiri unakuta imejaa. Sasa nenda Airtanzania Unaweza kukuta imejaa; ukienda kusafiri ina 65% kwa treni nilikuwa nilikuwa sijafuatilia ila inaonekana kama hali ni hiyo hiyo

Swali ni je? kwa nini mashirika ya private au ya kimataifa yanayotumia hiyo mifumo yanajaa?
AU basi niseme wanatakiwa wafanye utafiti kwa nini hiyo hali inatokea na sio kutoa tu majibu ya kimazoea..ULIMWENGU UMEBADILIKA ...UNATAKA SOLUTION NA SIO MAJIBU....LAKINI PIA KUACHA ABIRIA SIO SIFA. Pengine waongeze option ya release seat any time within 24hrs before travel (ili ziuzike tena)
Ninapanda treni kila mwezi, hili jambo la seat kuwa empty wakati walisema imejaa naliona mara nyingi
Mda mwingine unawaza kwamba watu watapanda mkifika Morogoro ila napo mkifika hola
 
Back
Top Bottom