Pre GE2025 Mbunge wa Ulanga: Hata nisiposhinda Uchaguzi mwaka huu, Rais Samia lazima ashinde

Pre GE2025 Mbunge wa Ulanga: Hata nisiposhinda Uchaguzi mwaka huu, Rais Samia lazima ashinde

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Hasham amesema kuwa kutokana na mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, hata kama hatapata tiketi ya ubunge, atahakikisha Rais Samia Suluhu Hassan anapata kura za kutosha katika jimbo hilo.

Salim ameyasema hayo wakati akieleza mafanikio mbalimbali yaliyoletwa na serikali katika maadhimisho ya miaka 48 tangu kuanzishwa kwa chama hicho.

Sherehe hizo kimkoa zimefanyika katika Kata ya Mwaya jimboni humo, ambapo amesema jimbo hilo lina vijiji 59, na hadi sasa vijiji 57 vimepata huduma ya umeme huku vijiji viwili vikikosa umeme.

Soma pia: Pre GE2025 Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Amesema hata ikitokea hajashinda ubunge, atahakikisha Dkt. Samia anapata kura za kutosha katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.


Source: Global Online TV
 
Back
Top Bottom