Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Hasham amesema kuwa kutokana na mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, hata kama hatapata tiketi ya ubunge, atahakikisha Rais Samia Suluhu Hassan anapata kura za kutosha katika jimbo hilo.
Salim ameyasema hayo wakati akieleza mafanikio mbalimbali yaliyoletwa na serikali katika maadhimisho ya miaka 48 tangu kuanzishwa kwa chama hicho.
Sherehe hizo kimkoa zimefanyika katika Kata ya Mwaya jimboni humo, ambapo amesema jimbo hilo lina vijiji 59, na hadi sasa vijiji 57 vimepata huduma ya umeme huku vijiji viwili vikikosa umeme.
Amesema hata ikitokea hajashinda ubunge, atahakikisha Dkt. Samia anapata kura za kutosha katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.