Mbunge wa viti Maalumu ana msaada gani kwa wananchi?

Mbunge wa viti Maalumu ana msaada gani kwa wananchi?

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
1,215
Reaction score
3,035
Salamu wana Jf
Matumaini yangu mama atausoma huu Uzi

Kuna mbunge wa viti Maalumu wa ccm jina kapuni,bungeni ajawahi kutoa hoja za kueleweka,tunaishi nae mtaa mmoja ni mama wa makamo hivi.baada ya kupata ubunge wa kusaidiwa ana dharau Sana hata salamu hatoi tutakutana 2025

Sehemu tulikuwa tunaishi Ina changamoto za barabara hasa kipindi Cha mvua barabara inakuwa chafu Sana.

Baada ya kukaa kikao tukakubaliana kila mtu achangie sh 5000 ili tuweze kurekebisha hiyo barabara sababu serikali ya mtaa ipo tu kimya, ikabidi tupite kila nyumba kwa ajili ya michango tunashukuru wakazi wa eneo lile wengi waelewa,michango ilienda vizuri na wazee wakupinga kwenye maendeleo hawakosi wanasema hiyo ni kazi ya serikali kutengeneza barabara sisi hela hatuna.

Baada ya michango kwenda vizuri tuliwachagua wakazi wa pale baadhi na wazee wa ccm.
wakaongee na mbunge ili hatusaidie nguvu,kwenye maboresho ya barabara Ile.


Kufika kwa mbunge Mana alikuwa likizo shughuli za bunge Amna saizi.
Alitoa majibu ya dharau awezi kutoa hela yake kisa kutengeneza barabara ya mtaa ule kisa tulimchagua diwani wa chadema.

Je ni haki kweri kwa kiongozi wa serikali unaefanya kazi bungeni za wananchi kutoa majibu hayo

Naomba kuwasilishaa...🙏
 
Hivyo ni vyeo vya kupeana tu ulaji. Habina tofauti na vile vya UDC, URC, nk.
 
Back
Top Bottom