Mbunge wa Viti Maalumu ang'ang'ania Bangi ihalalishwe

Nilikutana na Afisa Mmoja tena mwandamizi..nikashangaa ananambia yule jamaa kipara alikuwa anatumie hichi kilevi.

Sikucomment chochote aisee!
 
Mbunge wa Viti Maalum Jaquelin Msongozi (CCM) amependekeza sheria ya Tanzania kuhalalisha bangi itumike kama Tumbaku.

Msongozi ametoa kauli hiyo leo Septemba 14, 2022 bungeni wakati akichangia muswada wa sheria ya Mabadiliko ya sheria mbalimbali namba 2 wa mwaka 2022.

Hata hivyo si mara ya kwanza hoja hiyo kutolewa bungeni kwani ilishawahi kutolewa na wabunge Jumanne Kishimba (Kahama), Joseph Msukuma (Geita Vijijini) na mbunge wa zamani wa Nkasi Kaskazini Ali Keisy.

Akichangia leo kwenye marekebisho ya sheria ya dawa za kulevya, mbunge huyo amesema Kuna Mataifa ambayo yaliruhusu bangi kwa faida yao na sasa wanaingiza Kodi.

"Tuige mfano wa Nchi kama Jamaica na Malawi, wenyewe wameruhusu bangi na sasa hakuna shida kwao, tuifanye ikubarike na kama Kuna shida tuandike tahadhari kama ilivyo kwa sigara,” amesema.

Mbunge huyo ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria amesema ikifanyika hivyo hata nchi inaweza kupata mapato.

Akijibu hoja hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Eliezer Feleshi amesema bado hakuna sheria ya kuruhusu bangi hasa kwenye biashara isipokuwa kuna sheria inaruhusu kama bangi inahitajika kwa kazi maalumu.
Bangi inauzwa Ulaya kama sigara tu huko kwetu afrika bangi ni haramu lohh majangaa kweli.

Bora hata angesema inatumika kwa ajili ya matibabu ya kifafa nk
Ila Hana elimu kabisa ya mmea yeye anajua inavutwa tu mshamba wa kusoma huyo
 
Ukiona polisi wanachoma au wanaharibu mashamba ya bangi basi jua kabisa kuna mamilioni ya shilingi yanachomwa au kuharibiwa.

Bangi kwanza sio bidhaa adimu yapo imepigwa marufuku. Kila mtaa na kila kona ya hii nchi bangi inauzwa na kuvutwa hadharani kama vile ni jambo lililohalalishwa.
Kwa maoni yangu acha watu walime bangi na pia watu waache wavute bangi ila kuwe na elimu ya jinsi ya kuitunia. Maana nadhani ukiitumia kidogo ni nzuri. Iuzwe kwenye vipimbo maalum vya gram kuanzia 15-25. Na mtu kwa siku avute gram 75 tu.
Legalize it, Marijuana......by Peter Tosh

Kweli
 
Sasa Mkuu hapo walikuwa wanajadili mabadiliko ya Sheria ya madawa ya kulevya ndio akatoa hoja yake. Wewe ulitaka azungumzie maji na Elimu kwenye jambo la madawa ya kulevya. Ujuaji mwingi huna lolote inalojua mpuuzi tu
We bwege kilamtu anauhuru kuchangia anachohisi sijaandika makalioni kwako.
Angeacha kuchangia upuuzi asubiri mada muhimu ndio aombe nafasi kuchangia. Muda wabunge tunaulipia so wasikae kutafuta kuwafurahisha ninyi wavutabangi uchwara!!!
 
Bhangi za uchochoron zimeshakuharibu ache ziuzwe pharmacy zitakusaidia
 
Bangi iruhusiwe wapiga kura tumechoka kuvuta kwa kujificha ficha huku tukiwasha washa udi, tumechoka.....
 
Wahalalishe tu wengine tuwe wakulima mabilionea .Waache ubinafsi.Huu uzi mzima umechangiwa na wavuta bangi[emoji1787]
 
Kalime wewe na familia yako.
Hili suala linajengwa, lilianza pale Hayati walivyoanza kufyeka mashamba... A pre-requsite to big money Investment Nina uhakika wapo watu wanaweza kuwa wamenza kiaina, tatizo linakuja kuwa ulimaji holela. Na ni wengi waliohaidiwa kuwa mabilionea....wanapigania.

Tuna madawa hatari kuliko hata bangi....mfano mzuri ni tarime. Wangapi walikufa na saratani maeneo hayo wakati wakisikika kuwa ni walimaji/wavutaji?
Kaja ACCACIA sasa saratani hiyo- kwa sababu za kemikali na madawa hatari.

Amini usiamini, kuna kipindi karibu niwaandikie kikosi kazi, wafanye storage za mbegu zote zilizopatikana katika sakasaka zao. Kuna treasure pale....mbegu ambazo hazijabadilishwa(genetics/modified). Tuna mbegu nzuri Karibu na Malawi. Vile vile kwa wale ambao wamelima miaka nenda rudi ndio wapewe kipaumbele(uzalendo) ni Wakulima wawezeshwe badala ya kuanza kutudanganya na kilimo kipya, ati waje wawekezaji. Tutaharibu.

Amani.
I second
 
Hata hivyo si mara ya kwanza hoja hiyo kutolewa bungeni kwani ilishawahi kutolewa na wabunge Jumanne Kishimba (Kahama), Joseph Msukuma (Geita Vijijini) na mbunge wa zamani wa Nkasi Kaskazini Ali Keisy.

Akichangia leo kwenye marekebisho ya sheria ya dawa za kulevya, mbunge huyo amesema Kuna Mataifa ambayo yaliruhusu bangi kwa faida yao na sasa wanaingiza Kodi.
Ametumwa na anaowawakilisha au bangi zimemtuma aseme hivyo?
 
Mbunge wa Viti Maalum Jaquelin Msongozi (CCM) amependekeza sheria ya Tanzania kuhalalisha bangi itumike kama Tumbaku.

Msongozi ametoa kauli hiyo leo Septemba 14, 2022 bungeni wakati akichangia muswada wa sheria ya Mabadiliko ya sheria mbalimbali namba 2 wa mwaka 2022.

Hata hivyo si mara ya kwanza hoja hiyo kutolewa bungeni kwani ilishawahi kutolewa na wabunge Jumanne Kishimba (Kahama), Joseph Msukuma (Geita Vijijini) na mbunge wa zamani wa Nkasi Kaskazini Ali Keisy.

Akichangia leo kwenye marekebisho ya sheria ya dawa za kulevya, mbunge huyo amesema Kuna Mataifa ambayo yaliruhusu bangi kwa faida yao na sasa wanaingiza Kodi.

"Tuige mfano wa Nchi kama Jamaica na Malawi, wenyewe wameruhusu bangi na sasa hakuna shida kwao, tuifanye ikubarike na kama Kuna shida tuandike tahadhari kama ilivyo kwa sigara,” amesema.

Mbunge huyo ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria amesema ikifanyika hivyo hata nchi inaweza kupata mapato.

Akijibu hoja hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Eliezer Feleshi amesema bado hakuna sheria ya kuruhusu bangi hasa kwenye biashara isipokuwa kuna sheria inaruhusu kama bangi inahitajika kwa kazi maalumu.
Wataitoa wapi kwa kazi maalum ikiwa kila uchwao inafyekwa kwa hiyo watatoa pesa ya wananchi kwenda kununua bangi kwa kazi maalum?
 
Back
Top Bottom