Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mbunge wa Viti maalumu Kigoma, Sabriana Sungura ameambatana sambamba na aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Wilfred Rwakatale kuhamia chama cha Wananchi CUF.
Aidha, katika katika shamrashamra za Wabunge hao kupokelewa katika Chama cha CUF, Mh. Sabriana Sungura amesema ameamua kujiunga na chama hicho kwa lengo kupata haki sawa na furaha baada ya kuikosa kwa muda mrefu katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA.
Amesem, katika chama hakukuwa na haki wala furaha badala yake kilitawaliwa na ubinafsi pamoja umimi.
” Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimetawaliwa na ubinafsi pamoja na umimi,kwani baada ya kufunga ndoa na mtu anayetoka katika Chama Cha Wananchi CUF nilinuniwa pamoja na kutegwa kwa madai kuwa natoa siri za chama,”amesema Sabrina.
Amesema kuwa, baada ya kuona hayo moja kwa moja kwa imani yake aliona jambo hilo ni la ubinafsi na kuamua kutazama pembeni.
Naye, Makamu Nwenyekiti wa CUF Bara, Maftah Nachuma, amesema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinashika dola pamoja na kurudisha heshima iliyokuwepo awali.
Amesema,ujio wa wabunge hao ni mzuri na umelenga kukifikisha Chama Cha CUF mbali kwa kuhakikisha itikadi ya haki sawa kwa wote inatekelezwa.
“Chama Cha CUF kimezaliwa upya Sasa kwa pamoja tunashiriki na kusimama imara kuhakikisha chama kinasonga mbele,”amesema Nachuma.
PIA SOMA - Wilfred Lwakatare arejea CUF baada ya kufutwa uanachama CHADEMA. Kutumika kuiangamiza CHADEMA