Mbunge wa viti maalumu CHADEMA, Sabriana Sungura ahamia CUF

Mbunge wa viti maalumu CHADEMA, Sabriana Sungura ahamia CUF

Naona upuuzi unaendelea, hata wakitongozwa huko mtaani watasema Mbowe.

Na wewe mleta mada dhaifu sana.
 
Alikuwa wapi toka ameolewa leo ubunge umekoma ndio aje kuongea kala pesa weee kashiba halafu anatafuta fursa mpya wachumia tumbo bwana.
 
Siko ccm wala chadema lakn tujiulize wote hao wanasema mbowe kawanyanyasa mbona sheria isichukue mkondo wake mpk sasa??? Na huko chadema rijali ni mbowe tu?? maana walijaribu mchafua kwa kula pesa wakaona hailipi wameamua amia kwenye unyanyasaji
 
CCM wanachekesha sana,baada ya kuona watu wamewashtukia wananunua upinzani wakaamua kuwafanyia shopping NCCR,baada ya watu pia kushtukia NCCR ni mpango wa kando wameamua sasa hivi kuwanunua na kuwahamishia CUF.

Hongera CCM,sasa hivi mmekuwa na wake watatu ,CUF,NCCR na TLP.

CUF ni mke mkubwa wakati wowote yupo hata umtende ,TLP ni mke wa pili,hapendwi ila analazimisha mapenzi ,mke mdogo ni NCCR mageuzi kwa sasa mapenzi yapo on fire
Money Stop Nonsense
 
View attachment 1463673

Mbunge wa Viti maalumu Kigoma, Sabriana Sungura ameambatana sambamba na aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Wilfred Rwakatale kuhamia chama cha Wananchi CUF.

Aidha, katika katika shamrashamra za Wabunge hao kupokelewa katika Chama cha CUF, Mh. Sabriana Sungura amesema ameamua kujiunga na chama hicho kwa lengo kupata haki sawa na furaha baada ya kuikosa kwa muda mrefu katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA.

Amesem, katika chama hakukuwa na haki wala furaha badala yake kilitawaliwa na ubinafsi pamoja umimi.

” Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimetawaliwa na ubinafsi pamoja na umimi,kwani baada ya kufunga ndoa na mtu anayetoka katika Chama Cha Wananchi CUF nilinuniwa pamoja na kutegwa kwa madai kuwa natoa siri za chama,”amesema Sabrina.

Amesema kuwa, baada ya kuona hayo moja kwa moja kwa imani yake aliona jambo hilo ni la ubinafsi na kuamua kutazama pembeni.

Naye, Makamu Nwenyekiti wa CUF Bara, Maftah Nachuma, amesema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinashika dola pamoja na kurudisha heshima iliyokuwepo awali.

Amesema,ujio wa wabunge hao ni mzuri na umelenga kukifikisha Chama Cha CUF mbali kwa kuhakikisha itikadi ya haki sawa kwa wote inatekelezwa.

“Chama Cha CUF kimezaliwa upya Sasa kwa pamoja tunashiriki na kusimama imara kuhakikisha chama kinasonga mbele,”amesema Nachuma.

PIA SOMA - Wilfred Lwakatare arejea CUF baada ya kufutwa uanachama CHADEMA. Kutumika kuiangamiza CHADEMA
WAMEHAMIA BAADA YA KUFUKUZWA ,WASIANZE CHOKOCHOKO HUKO CUF
 
Huyo hakufuata chama kwa hiyari na mvuto bali kamfuata mume wake, kwa kifupi ‘KULINDA NDOA’! Aache kuzunguka mbuyu, simply say the truth and ashame the devil, IQ!
Sasa wote wakufeli ubunge Nani atawasomeshea watoto?,maana uchaguzi huu kwakweli hautabilika,Kuna watu wako na mtimanyongo,wametulia tuli Kama hawapo vile
 
Tunataka kiongozi mwenye kutetea watu wake nasio kuwanyanyasa kama afanyavyo mbowe

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo jiwe ni damu tupu za wananchi WA nchi hii na haijtokeapo kwa awamu zilizopita na hukemei na ushahidi upo WA kutosha. Mbowe awe amefanya hayo mnayomuazia awe hajakamatwa na kufungwa ni serikal yenu. Hebu ukila mda mwengine hayo masikio yapitishie tonge moja moja yapanukee.
 
Wenye akili kitambo tulisha wadharau Chadema.
 
Back
Top Bottom