Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM), amewataka wanachama wa chama chake kuacha kumwekea fitna ili apate fursa ya kugombea tena ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi ujao. Akizungumza nje ya viwanja vya Bunge na Jambo TV, Waitara alieleza kuwa fitna hizo zinamwathiri na zinampa ugumu kupambana na mpinzani wake mkuu, John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, anayetarajiwa kuwania nafasi hiyo.
Waitara amesisitiza kuwa anahitaji mazingira ya haki ndani ya chama chake ili kutumia nguvu kupambana na wapinzani kutoka vyama vingine. Amesema vitisho na matukio ya utekaji dhidi ya wafuasi wake ni dalili za siasa chafu, akitaja utekaji wa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Itirio, Mhere Magaho, pamoja na kada wengine, Mwita Gati na Marwa Isare, usiku wa Februari 9, 2025.
Waitara amehusisha matukio haya na siasa za ndani ya chama, akidai wafuasi wake wanatishwa kuacha kumuunga mkono.