Pre GE2025 Mbunge Waitara: Tutapitisha miswada yote kwa kutumia wingi wetu

Pre GE2025 Mbunge Waitara: Tutapitisha miswada yote kwa kutumia wingi wetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Waitara anajihisi hatia ndani ya moyo wake, anajitaidi sana ili apate kukubalika ndani ya chama lakini wapi.

Waitara tumia vizuri mafao yako maana nina uhakika hautatoboa ktk uchaguzi ujao maana hauna faida yoyote kwa chama chako, jimbo lako na nchi kwa ujumla
Atawekwa kwenye dust đź—‘ bin !
 
Kwenye kikao cha bunge cha Februari 1, 2024, mbunge nyangarakasha Mwita Waitara alitamba bungeni mbele ya wabunge wenzake waliokuwa wakimshangilia kuwa wabunge wa CCM watatumia wingi wao kuipitisha miswada ya uchaguzi!

Swali, Tanzania ni mali ya nani, wabunge wengi wa CCM au wachache wananchi? Je, CCM bado inaendelea na "hii nchi ina wenyewe na wenyewe ni CCM"!
Siyo kwa kutumia akili na maslahi ya wananchi ila kwa kutumia wingi.
Naona aibu mimi,maana yake watu wanafuata Mkumbo si umuhimu wa hoja.
 
Kwa wale wasiofahamu maana ya "kutumia wingi wetu", ni kuwa miswaada haitajadiliwa bali itapitishwa kama ilivyo.
Bahati mbaya kuna watu ambao hawaoni manufaa ya kuijadili miswaada wao wanadhani ikijadiliwa Chadema watanufaika! Hao ni akina Lucas Mwashambwa.
 
Kwanza hili Bunge wabunge wenyewe ni wa mchongo hivyo hatushangai.

Magu katuharibia sana hii nchi kwa kuua taasisi muhimu kama Bunge.
Liliharibika sababu sisi ndio tulitaka linaribike. Tusingetaka lisingeliharibika. Sasa hii ya kujitapa kupitisha hata uchafu ni nini sasa?
 
Kwenye kikao cha bunge cha Februari 1, 2024, mbunge nyangarakasha Mwita Waitara alitamba bungeni mbele ya wabunge wenzake waliokuwa wakimshangilia kuwa wabunge wa CCM watatumia wingi wao kuipitisha miswada ya uchaguzi!

Swali, Tanzania ni mali ya nani, wabunge wengi wa CCM au wachache wananchi? Je, CCM bado inaendelea na "hii nchi ina wenyewe na wenyewe ni CCM"!
Waitara ame changanyikiwa. 2025 itakuwa.mwisho wa kusikia jina lake.
 
Waitara ame changanyikiwa. 2025 itakuwa.mwisho wa kusikia jina lake.
Utaratibu wa kupiga kura ni ule ule ambao CCM wanaandaa, wanasimamia, wanatangaza mshindi kisha wanamalizia kwa kuhesabu kura!
 
Kutokana na wingi wao wamepitisha miswaada yote mitatu bila mjadala.
 
Back
Top Bottom