PreGE2025 Mbunge Wanu Ameir afungua mafunzo kuwajengea uwezo Viongozi na Watendaji wa UWT

PreGE2025 Mbunge Wanu Ameir afungua mafunzo kuwajengea uwezo Viongozi na Watendaji wa UWT

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
WhatsApp Image 2025-04-20 at 13.28.36.jpeg


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusingi Unguja, Mhe. Wanu Hafidh Ameir amefungua mafunzo elekezi kwa viongozi na watendaji wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuanzia ngazi ya Matawi, Wadi, Jimbo na Wilaya yaliyofanyika kwenye ukumbi wa TASAF, Zanzibar

Wanu amefungua mafunzo hayo tarehe 20 Aprili, 2025 yenye lengo la kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wa UWT hasa kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapoelekea kushiriki uchaguzi mkuu wa kuchagua Rais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani nchi nzima ifikapo mwezi Oktoba, 2025.

Akuzingumza katika mafunzo hayo, Mhe. Wanu Ameir amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha viongozi hao wa UWT ngazi zote kukumbuka wajibu wao hasa CCM inapokuwa kwenye uchaguzi na kupanga mipango ya ushindi

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mhe. Wanu Ameir amewasisitiza wanawake kuwa wasisite kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi za uongozi wa dola nchini kwani Wanawake wanaweza lakini ni lazima kwanza wathubutu kwa kuonesha nia ya kuwatumikia wananchi

Mwisho, Mhe. Wanu Ameir amewapongeza viongozi na watendaji wote wa UWT kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mafunzo hayo kwani hii imeonyesha wazi kuwa UWT wako tayari kujifunza ili kuongeza ufanisi katika majukumu yao.

WhatsApp Image 2025-04-20 at 13.28.37.jpeg
 
Bungeni mchango ni sifuri, kazi kugonga meza tu, huyu atafundisha kitu gani?
 
Keshokutwa tu tutasikia naye amekuwa rais kama mama yake
 
Back
Top Bottom