PreGE2025 Mbunge Wanu Ameir Akabidhi Kisima cha Maji Makunduchi, Zanzibar

PreGE2025 Mbunge Wanu Ameir Akabidhi Kisima cha Maji Makunduchi, Zanzibar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Wanu Hafidh Ameir jana tarehe 22 Machi, 2025 amekabidhi kisima cha maji katika Kijiji cha Miwaleni Makunduchi kitakachosaidia kutatua changamoto ya maji kijijini hapo.

WhatsApp Image 2025-03-23 at 16.04.25.jpeg
Itakumbukwa kuwa, jana tarehe 22 Machi, 2025 ilikuwa ni siku ya kuadhimisha Wiki ya Maji Duniani (World Water Day) iliyokuwa na Kauli Mbiu: Uhifadhi wa Uoto wa Asili kwa Uhakika wa Maji

Kwa upande wake, Wanu Hafidh Ameir amesema kuwa, amekabidhi kisima cha maji ili kiwe kama sadaka kwa wakazi wote wa Kijiji cha Miwaleni Makunduchi ili kuwatoa watu katika shida na dhiki ya kuhangaika na maji.

Aidha, Wanu amesisitiza wananchi kuwa na utunzaji mzuri wa vyanzo vya maji sambamba na matumizi sahihi ya miundombinu ya maji ili miundombinu iendelee kunufaisha wananchi kwa muda mwingi

Vilevile, Wanu amesema kuwa, ataendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji kijijini Miwaleni Makunduchi na maeneo mengine na kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama ili kuwa na afya bora

Mwisho; Wananchi wa Makunduchi wamemshukuru Mwenyekiti wa MIF, Mhe Wanu kwa kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwatumikia kwani miradi mingi ya maendeleo imewafikia katika kipindi cha uongozi wake, ikiwemo miradi ya sekta ya maji

WhatsApp Image 2025-03-23 at 16.04.27.jpeg
 
Kwa wasiomjuwa huyo Wanu ni mtoto wa Mama Samia Suluhu Hassani.

Hafidh ndio first gentleman, mume wa Mama Samia.

Mchengerwa naye kaowa mtoto wa Mama Samia kawekwa Tamisemi yuko ofisi ya Rais.

Halafu wewe mla makande unashabikia ccm bila kujuwa hicho chama kina wenyewe.
 
Wandele Mbona Wamenyong'onyea,,Wana Huzuni,,Wamenuna Hivyo Au Swaumu.
 
Back
Top Bottom