Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mbunge Damas Ndumbaro karudi jimboni kwake Songea leo kuwasalimia wananchi wake miaka mingi imepita tangu achaguliwe ubunge.
Mbunge huyu katoa zawadi, kaongozana na wataalam na watu wengine wengi tu muda alowakusanya haujulikani akiwa na msafara wa magari yasozidi 10!
Je, Mbunge huyu aweza kutatua tatizo lolote jimboni kwake miezi zaidi ya mwaka imebakia ufanyike uchaguzi mkuu ujao wa 2025?
Jimbo lake la Songea Mjini halina barabara za lami na pia kata ya Mletele hadi Mdundiko hakuna maji , je wananchi hawa wamekuwa wakioga wapi, kutawadha wapi na kunywa maji yepi?
Pia tatizo la barabara limewafanya wananchi wawe na wakishindia pombe kwa kukosa shughuli za kufanya za kiuchumi (mobility issues) jambo linodumaza maendeleo ya jimbo hilo.
Mbunge Damas Ndumaro hafaikabisa kuendelea kuwa mbungewa jimbo hilo baada ya miaka migni kupita jimbo halina maji wala barabara nzuri ya lami. Na kutoa kiasi cha fedha 500k hakutasaidia chochote kukamilisha utandazaji wa bomba la maji kutoka Mdundiko hadi Mletele.
Wananchi wana haki ya msingi kabisa ya kutomchagua mbunge huyo na badala yake wachague watu mbadala na kama hawapo basi wananchi hao wasipige kura.
Je, ni Makonda na Silaa ndo walowakumbusha wabunge kama Ndumbalo kuanza kwenda majimboni kwao kusikiliza shida za wananchi wao walowachagua miaka minne au mitano ilipita?
Chondechonde wananchi tuamke mbunge anapoingia jimboni kuanzia sasa hivi na hajafanya chochote basi asichaguliwe ili kuwafunza wabunge hao kwamba wanawajibika kuwepo bungeni kila mara.
Pia kuanzia sasa ni vema wabunge wote wakawa na ofisi (surgery) kwa ajili ya kuonana na wananchi wao wenye shida na matatizo mbalimbali.
Na fedha za kujengea ofisi zao zitokane na malipo yao wenyewe ambayo hukunja na kubakia nje ya majimbo yao.