Pre GE2025 Mbunge yeyote anayerudi jimboni leo miaka zaidi ya 5 imepita kutembelea jimbo asichaguliwe tena

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni njia ipi sahihi ya kumuondoa Mbunge ambae hajafanya chochote bungeni kwake zaidi ya miaka 5 imepita?

Je ni kura ya maoni?
 

Katika sababu hizo tatu wananchi wana muda wa kuwafikiria wagombea ubunge wao kwa kuangalia sababu ya tatu (Issue Voting)yaani masuala ya kupiga kura kulingana na sababu mbalimbali ikiwemo mbunge amefanya nini bungeni.

Hiyo ni kwasababu tayari wananchi (kwenye factors mbili za mwanzo) wana ukaribu mno na chama cha mgombea au binafsi wanamhusudu hivyo hata kwa mabaya yake.

Hilo ndo la kuliondoa.
 
Kazi ya mbuzi ni kuchagua mbuzi mwenzao hivyo usishangae wakimchagua.
 
Wangoni na ccm ni kama samaki na maji. Huwambii kitu.
Sijui kama watakuelewa.
 
Wangoni na ccm ni kama samaki na maji. Huwambii kitu.
Sijui kama watakuelewa.
Tena kukiwa na shughuli huhamia mjini kutoka majumbani mwao.

Kazi kwelikweli, lakini ni ile genereation ya zamani ndo shida na ndo wenye ushawishi.

Kizazi cha sasa chahitaji elimu tu ya mpiga kura na haki zake pamoja na wajibu wake.
 
Inatakiwa kuwa hivyo. Ila wadanganyika tuna MATATIZO. Subiri utaona!
 
Viongozi wa ccm wenyewe wanakuambia upinzani wao upo kwenye chama chao tu,akipitishwa chamani basi huku kwingine akumsumbui!
 
NAMI naongezea.
Ingewekwa Sheria Ili uweze kugombea ubunge, uwe unaishi/ umeishi Jimbo husika siyo chini ya miaka 10 mfululizo. Uwe na nyumba na wewe na familia Yako uishi Jimbo husika kwa kipindi tajwa hapo juu.
Ilivyo Sasa mtu anatoka huko anakuja kugombea hata hajui mahitaji ya wana Jimbo,hajawahi kushiriki MATATIZO ya kijamii,wananchi wana changamoto gani hajui halafu anapewa NAFASI ya kutatua changamoto ambazo hazijui.
 
Dr Damas buanaaa ana dhihaka sanaaa......hakuwa chaguo la wana Sonfea alitolewa huko number 6 ....akawa no 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…