Mbunge Zaytun Swai akemea vitendo vya ukatili wa kijinsia - Mkoa wa Arusha

Mbunge Zaytun Swai akemea vitendo vya ukatili wa kijinsia - Mkoa wa Arusha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mhe. Zaytun Swai ametoa salamu za pongezi kwa WanaCCM katika hafla ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Halima Mamuya.​

Mhe. Zaytun Swai amempongeza Ndugu Halima Mamuya na amesema ni heshima kubwa kwa wanawake wa Tanzania na kwa Wanawake wa Mkoa wa Arusha.

"Nina imani kwa pamoja tunaweza kuendelea kukijenga Chama Cha Mapinduzi kwa Mkoa wa Arusha kwa uwepo wa Ndugu Halima Mamuya" - Mhe. Zaytun Swai

"Sasa hivi Dunia yetu inakabiliwa na janga la ukatili wa kijinsia, ulawiti na ubakaji wa watoto. Ninawaomba viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Serikali, Viongozi wa Dini kwa pamoja tuendelee kushirikiana kukomesha ukatili wa kijinsia, ubakaji na ulawiti kwa watoto wetu" - Mhe. Zaytun Swai

"Hili suala ni suala letu wote, kama jamii tukishirikiana naamini tunaweza kujikwamua. Kila mmoja wetu akisimamia malezi bora kwenye Kaya zetu na kwenye maeneo yetu yote ambapo tumetoka tutaweza kutokomeza ukatili wa kijinsia wa ubakaji na ulawiti kwa watoto wetu" - Mhe. Zaytun Swai
WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.39.28(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.39.27.jpeg
WhatsApp Image 2023-02-26 at 16.39.28.jpeg
 
Back
Top Bottom