Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
MBUNGE ZUBERI KUCHAUKA ASHAURI TATHIMINI IFANYIKE GHARAMA ZA KUUNGANISHWA UMEME
Mbunge wa Jimbo la Liwale mkoani Lindi, Zuberi Kuchauka ameishauri Serikali kupitia Wizara ya Nishati kufanya tathmini kuhusu gharama za kuunganisha umeme kwa wananchi kwa kuangalia uwezo wao wa kifedha na sio kuangalia miji au vijiji wanapoishi akitoa sababu kuwa kuna watu wapo mjini lakini hawana uwezo mkubwa na wengine wapo kijijini lakini wana uwezo mkubwa.
Kuchauka amesema hayo leo Aprili 28, 2025, wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
"Liwale kule kwetu hatuna miji, kule kuna vijiji. Sasa unamwambia mwanakijiji wa pale Liwale mjini eti kwa sababu yupo mjini, mnaita vijiji miji kwamba alipe shilingi 350,000/- wakati wenzake wa vijijini wanalipa shilingi 27,000/- kidogo kuna kigugumizi"
"Wapo wakulima vijijini wamepata fedha za korosho wamejenga majumba makubwa mpaka ma 'pub' yapo kule lakini kuingiza umeme anaingiza kwa shilingi 27,000. Mwenzangu na mimi mjini pale amegalagala amepata zake shilingi 200 amejenga vyumba vyake viwili, kuingiza umeme 350,000/-" amesema Kuchauka