TANZIA Mbunifu wa jina la Tanzania, Mohammed Iqbal Dar afariki Dunia nchini Uingereza

TANZIA Mbunifu wa jina la Tanzania, Mohammed Iqbal Dar afariki Dunia nchini Uingereza

Mzee Dar ndio alituna jina Tanzania na pia Sir name yake ndio imeunda jina Dar es Salaam.

R.I.P

View: https://www.instagram.com/p/DGxhMTOIEzM/?igsh=MWNndWdvMDBic2JjMw==

Pumzika kwa amani Muasisi.
Kwanini watu wa namna hii tunafahamishwa habari zao mara nyingi pindi wanapo aga dunia ?

Ni vema watambulishwe public kwa uthubutu wao unao acha alama inayoishi katika nchi wakati wote wa uhai wao na hata baada ya.

Waandishi na wenyetaaluma ya habari, Makala zenu pia ziangazie watu kama Bwana Dar. Historia ya Taifa itakuwa hai.

Hov.
 
Unakuta hata kwenye Vitabu vya historia hawapo ila wamejiweka Wanasiasa wapuuzi wapuuzi tuu wasio na maana.

Huyo alitakiwa apewe hata mtaa
 
Unakuta hata kwenye Vitabu vya historia hawapo ila wamejiweka Wanasiasa wapuuzi wapuuzi tuu wasio na maana.

Huyo alitakiwa apewe hata mtaa
Sahihi sana. Hapo kwenye Mtaa ni Moja ya Legacy reflectory Bar makini.

Hapa wana habari wanagap la kufanya kazi.
 
Binadamu aliyebuni jina la taifa la Tanzania, Mohanmmed Iqbal Dar, amefariki Dunia akiwa usingizini jijini Birmingham, Uingereza alikokuwa akiishi akiwa na umri wa miaka 80.

Mohammed Iqbal Dar aliyezaliwa Agosti 8, 1944, mjini Tanga, alikuwa mtoto wa Dk Tufail Ahmad Dar, daktari maarufu aliyehudumu katika mikoa ya Tanga na Morogoro nchini Tanzania. Mwaka 1965 alihamia Uingereza alipokuwa akiishi hadi kifo chake.

Igbal alishiriki katika shindano la kutafuta jina la Tanzania lililoandaliwa mwaka 1964 kabla ya Muungano ambako yeye alikuwa mmoja wa wanafunzi 80 walioshindana na hatimaye yeye kuibuka mshindi.

Akizungumzia jinsi alivyobuni jina TANZANIA enzi za uhai wake Iqbal alisema alichukua herufi tatu kutoka jina la nchi ya Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar nikachukua herufi tatu za mwanzo ZAN, kisha nikaunganisha nikapata jina TANZAN.

Baada ya hapo alichukua herufi ya kwanza ya jina lake ‘lqbal’ kisha akachukua herufi ya kwanza A ya jina la dini yake yaani Ahmadiya na kuunda jina TANZANIA.

lqbal ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 18 alishinda shindano la kupendekeza jina moja litakalozitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar na kupewa zawadi ya shilingi mia mbili (Tsh 200/=) za wakati huo.
 
Attachments

  • 1741101542854.jpg
    1741101542854.jpg
    306.7 KB · Views: 1
  • 1741101542854.jpg
    1741101542854.jpg
    306.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom