Mbute: chakula kinachotokana na mihogo

Mbute: chakula kinachotokana na mihogo

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Mbute ni chakula kinachotokana na zao la muhogo ambao humenywa na kuvundikwa kwa maji halafu huchemshwa.

Chakula hicho huwa kitamu kupita muhogo uliopikwa.

Maandalizi ya mbute
Mbute hutokana na zao la muhogo ambapo humenywa na kuanikwa kwa muda halafu huvunda kwa muda. Baadaye huchukuliwa na kupikwa hadi huwa tayari kuliwa.mbute huweza kuliwa kama chakula cha asubuhi, mchana pia hata jioni chakula hiki huweza kutumiwa na watu wa lika lote wakiwemo watoto, vijana pamoja na wazee.

Matumizi ya mbute
Mbute hutumika kwa ajili ya chakula kwa mwanadamu hususani katika jamii za kiafrika kama kabila la Wasukuma kwenye Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora, Simiyu na Geita nchini Tanzania. Zao hili la muhogo ulio vundikwa hujulikana kwa jina la mbute ambapo huwa ni muhogo ulio kwisha kumenywa na kukaa kwa muda kwa ajili ya matumizi ya baadae kabla ya kuvundikwa na kuwa mbute maalumu kwa ajili ya chakula.
 
Mbute tamu sana jina jingine ni makopa
 
Kuhusu mbute umenikumbusha siku Moja hivi mshua alitupa task ya kusesa majani nyuma ya choo back then ilikua 90s.
Tulikua mimi na brothers wangu wawili jumla wa 3 including me. Katika kufanya ile task tukabahatika kukutana na shilingi 50 Ikiwa na kutu kinoma.
Kwa sababu nilikua mdogo brothers walinipa kitengo cha kuitakatisha ile 50 mpaka ing'ae, ili iweze kukubalika kupokelewa wakati wa manunuzi.
Nilikomaa nayo sugua chini kuwa kisingino mixer kuisugua kwenye daladala yani kiufupi niliwekeza muda na ubunifu wa kutosha kwenye kuitakatisha ile shilingi 50.
Mungu si athumani mzigo ila ng'aa kwa kadri ya uwezo wangu.
Long story short ni kwamba ile shilingi 50 tui-escort sisi wote wa3 kwenda soko la jioni kununua Mbute Moja hiyo kubwa mno kimo cha buti la jeje.
 
zipo mbute za kuchoma na kupikwa ila hivi vitu hua navipenda sana.

Sema ndio hivyo kwa sasa kuvipata ni nadra sana.
 
Back
Top Bottom