Mbuyu Twite,Obrey Chirwa out Yanga,Jesse Were,Meshack Chaila in!!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
KOCHA mpya wa Yanga, George Lwandamina amependekeza wachezaji wawili wasajiliwe dirisha hili dogo, ambao ni kiungo wa ulinzi Mzambia Meshack Chaila na mshambuliaji Mkenya Jesse Were.
Chaila na Were wote walikuwa wachezaji tegemeo wa kocha Lwandamina katika kikosi cha Zesco United kilichofika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu kabla ya kutolewa na Mamelodi Sundwons ya Afrika Kusini iliyofanikiwa kutwaa taji hilo.

Na baada ya Lwandamina kuhamia Yanga, moja ya nafasi ambazo ameona zinahitaji marekebisho ni kiungo cha ulinzi na ushambuliaji na wachezaji sahihi kwa nafasi hizo kati ya wote aliokuwa anafanya nao kazi Zesco ameona ni Chaula na Were.Wakati huo huo watoto wa jangwani Yanga wamemalizani na kiungo fundi "kinda" mkabaji wa Mbeya city Raphael Alpha.
 
Angalau kwa Yanga naona muelekeo.
Mabadiliko ambayo sikuyapenda ni ya AZAM kuwaleta WA-HISPANIA.... sidhani kama itapiga hatua yoyote mbele
 
Angalau kwa Yanga naona muelekeo.
Mabadiliko ambayo sikuyapenda ni ya AZAM kuwaleta WA-HISPANIA.... sidhani kama itapiga hatua yoyote mbele
Yanga wanamuelekeo gani zaidi ya kila kitu kuwaiga watani wao wa jadi. Hii yote ni jinsi simba ilivyo chini ya omog. Kesho simba nendeni spain mkalete kocha muone kama vyura nao hawajaenda huko
 
Yanga wanamuelekeo gani zaidi ya kila kitu kuwaiga watani wao wa jadi. Hii yote ni jinsi simba ilivyo chini ya omog. Kesho simba nendeni spain mkalete kocha muone kama vyura nao hawajaenda huko
Kama wanawaiga katika mazuri kuna tatizo gani?
Mbona katibu na kocha wa simba wote walikuwa AZAM na husemi?
 
Yanga wanamuelekeo gani zaidi ya kila kitu kuwaiga watani wao wa jadi. Hii yote ni jinsi simba ilivyo chini ya omog. Kesho simba nendeni spain mkalete kocha muone kama vyura nao hawajaenda huko
Duh! Hata kuleta Pluijm Yanga wameiga Simba?

Ni lipi Yanga wameiga Simba?
 
Kama wanawaiga katika mazuri kuna tatizo gani?
Mbona katibu na kocha wa simba wote walikuwa AZAM na husemi?
Yanga wanaboresha kikosi kwa ajili ya kuleta ushindani kwenye michuano ya Kimataifa.

Simba wanaboresha kikosi kwa ajili ya kufanya vyema LigiKuu...

Mtu anakuambia... Ohhh Yanga wanaiga simba!!!
 
Kipigo cha LIBORO kina watokea usingizini... Simba watani wa jadi bishana na ndanda. Stand... Yanga ya kimataifa 25 November wanakwa pipa ulayaaa... Nyie nendeni Ethiopia mnatangazaa.. Yanga timu bora afrika mashariki katika ranks za CAF.... Mwakani mechi zote za CAF Mwanzaa
 
Watakuwa wamefanya makosa makubwa Chirwa bado ana umri mdogo, and is very promising player. Wakuacha hapa walikuwa Tambwe /Niyonzima na Twite. Tambwe hana msaada wowote katika mechi za kimataifa, Niyo umri umekwenda na ni mchezaji wa kufurahisha watazamaji. Hii game moja haiwezi kufuta makosa yake. Kama kweli ni haya mtakumbuka uzi huu.
 
Yanga wanamuelekeo gani zaidi ya kila kitu kuwaiga watani wao wa jadi. Hii yote ni jinsi simba ilivyo chini ya omog. Kesho simba nendeni spain mkalete kocha muone kama vyura nao hawajaenda huko

...Wa matopeni umenichekesha sana especially hapo kwenye red font. Eti kila kitu kuiga kwa mtani. Sasa je Kombe la FA, Ubingwa wa VPL na kuingia hatua ya makundi Klabu bingwa tumeiga kwenu pia?..
 
Duh! Hata kuleta Pluijm Yanga wameiga Simba?

Ni lipi Yanga wameiga Simba?

Kitu pekee Yanga anachoiga Simba ni kuwachukua wachezaji wao. Watapiga kelele mwisho wanatulia tulii. Angalia ya Yondani, Twite na sasa Kessy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…