Mbwa jamii ya Rottweiller waua mwangalizi wao Dar

Labda nijaribu kumsaidia mtoa mada sikuwepo eneo la tukio lakini nipo sana jirani na tukio lilipotokea na majirani walinipa dodoso ingawa sikufika,

1. Baba mwenye nyumba hakuwepo nyumbani alikuwa amesafiri siku ya tukio ni mama na kijana wa kazi walikuwepo nyumbani unajua wakina mama wanavyoogopa hawa wanyama.

2. Nikiwa nimelala mida ya saa 7 usiku nilianza kusikia milio ya risasi, kwa uzoefu wangu mdogo wa milio ya risasi nikajua kabisa hiyo ni silaha ndogo bastola less than 9mm, baadae kama saa 7.30 nikaanza kusikia milio ya shortgun hii ni silaha kubwa kidogo ambayo inatumiwa na walinzi wa makampuni binafsi, nikajua ni majambazi na askari wanarushiana risasi nikamwambia masai (mlinzi) wangu akae tayari.

3. Kufikaa saa 8 usiku nikasikia mlio wa SMG (Sub Machine gun) mlio haswa nikasema hili leo balaaa.

4. Nikampigia tena masai wangu mlinzi saa hiyo hiyo akiwa kajificha kichakani anasema pia anasikia sauti ya mtu analia sana , nikajua labda jambazi mmoja kajeruhiwa.

5. Baadae nikapata stori kwamba, baada ya mama mwenye nyumba kushindwa kuwamudu wale mbwa na silaha ndogo, aliwaita walinzi wa makampuni binafsi lakini baada ya kuona lile tukio wale askari wa kampuni binafsi wakasema wao hawawezi tumia short gum kuua wale mbwa kwa sababu risasi za short gun zinasambaa zinaweza mletea madhara yule kijana pia wakachemsha, nahisi walijaribu hata hatuwezi jua labda pia zilimpata, mida kama ya saa 9 kasoro polisi wakaitwa ndio wakaja na SMG wakapiga ule mlio mkubwa niliusikia kuwatawanya mbwa ndio baadae wakawapiga risasi na silaha ndogo.

6. Inaonekana mbwa wale walizoea milio ya silaha ndogo kwa hiyo walikuwa hawashtuki kwa wakati ule

7. Binafsi mimi nafuga mbwa lakini bado sipati picha kama watu wote waliogopa kujitosa kumuokoa yule mtoto pamoja na majirani wakiwepo kushuhudia. Kama unafuga mbwa na unaona huwezi kumcontrol bora uza.
 
Hawa mbwa ni hatari sasa wakikuta Mhehe si ndo wanamshambulia kwa hasira sana?
 
HV mnanjua Pitbull nyie...huyo rotywear cha mtoto kabisa
 
Nashukuru kwa kuongezea nyama kwa namna navolijua tukio, kujitosa kumwokoa pale ilitakiwa mbinu na si ujasiri. Make wale viumbe walishapata harufu ya damu, hivo yeyote ambaye angeingia kichwa kichwa ilikuwa iwe halali yao.

Pia hujagusia kipengele kwa nini hawa mbwa wamshambulie huyo ambaye alikuwa anawahudumia?

Swali la kichokozi je mwenye nyumba akisafiri anakambidhi mama bastola?
Hitimisho, nashukuru kwamba nawe umehitimisha kwamba handler alishindwa kucontrol, owner naye kashindwa, kampuni ya ulinzi nayo ikashindwa, mwisho wakaitwa polisi
 
Hapa navuta picha ningekuwa Ni Mimi ningewapasua vichwa hao makoko wote mmoja mmoja.
Kwamba unakamata mmoja unanyanyua juu na kubwaga chini au kupigiza ukutani.



Ila mnaofuga Hawa wanyamapori sijui huwa mnawaza nini
 
Hapa navuta picha ningekuwa Ni Mimi ningewapasua vichwa hao makoko wote mmoja mmoja.
Kwamba unakamata mmoja unanyanyua juu na kubwaga chini au kupigiza ukutani.



Ila mnaofuga Hawa wanyamapori sijui huwa mnawaza nini
Mbwa mwitu ndio mnyama pori ila Mbwa ni rafiki mkubwa sana wa binadamu ukijua kumhandle
 
Siyo lazima Sana kujibu hilo swali mkuu, Samahani
Nauliza hivyo nikiwa na sababu mkuu. Kuna jirani yetu aling'atwa na mbwa hao akalazwa hospitali. Hatujui hatma yake ndio nauliza huenda akawa yeye..
 
Ni wapi huko mkuu...
 
HV mnanjua Pitbull nyie...huyo rotywear cha mtoto kabisa
Sijawahi experience mbwa wote, ila kwa mujibu Kennel tofauti. Kila Mbwa ana sifa zake. Kwa list ya ubora wote anaanza German Shepherd akifuatiwa na Rottweiler hasa kwa upande wa intelligence na security
 
Nauliza hivyo nikiwa na sababu mkuu. Kuna jirani yetu aling'atwa na mbwa hao akalazwa hospitali. Hatujui hatma yake ndio nauliza huenda akawa yeye..
Ninaye mungelea hajalazwa mahali popote
 
Kaka swala la silaha ni la ndani, hujaona kesi mtoto anakutwa na silaha ya baba na anafanya nayo tukio, hayo ni mambo ya ndani sana, mke ni mtu wa karibu sana kuwa na silaha yako kulingana na tukio ana haki kisheria kutumia silaha yako kuokoa uhai wa mtu. Hii hata mahakamani anashinda kama ndivyo ilivyokuwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…