casanova69
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 2,361
- 2,166
Yani nifuge mbwa kwa ajili ya ulinzi alafu nimnunulie na kitenesi cha kuchezea?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yani nifuge mbwa kwa ajili ya ulinzi alafu nimnunulie na kitenesi cha kuchezea?
Labda nijaribu kumsaidia mtoa mada sikuwepo eneo la tukio lakini nipo sana jirani na tukio lilipotokea na majirani walinipa dodoso ingawa sikufika,KakaMkubwa... sikuwa na lengo la kukukomoa bali elimu uliyotoa imekaa poa na binafsi nimeipokea vizuri tu na ndomana hata comment zangu ukicheki nimeonelea ili kumwepuka mnyama huyo hatari basi bora kufuga wanyama wakali wa porini ujue moja tu kuliko kufuga mbwa anayetambulika ni wa nyumbani lakini masharti yake ni zaidi ya simba au zaidi ya mke mdogo!!!
Najua hii ni habari tu na hata wewe umefanya kuipata kutoka chanzo fulani cha habari ila nilichokuwa natafakari ni namna ilivyoripotiwa kutoka huko kwenye chanzo kwamba wameshindwa fulani na fulani mpaka akaja fulani ndo aka... kitu ambacho hakiniingii akilini kwavile spidi ya wanyama wenye kucha katika kushambulia sidhani kama kuna asiyeijua
Chukulia tu mfano chui mmoja anashambulia watu kadhaa ndani ya muda mchache sana watu wote chali halafu urudi kuvuta picha mbwa (tena wanne) washambulie mtu mmoja lakini kuchukue kitambo kiasi kwamba ipatikane time ya kuita watu tofauti tofauti na kwa muda tofauti.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kwahio ukinunua suti mpya lazima ukamuoneshe kwanza au??
Hawa mbwa ni hatari sasa wakikuta Mhehe si ndo wanamshambulia kwa hasira sana?Wana jamvi niwasalimu kwanza, na moja kwa moja niende kwenye mada.
Asubuhi ya leo nimepokea taarifa toka kwa rafiki yangu mmoja aliyeko Dar akitaka kufahamu kwa nini mbwa jamii ya Rottwieler hugeuka na kushambulia wamiliki na kufikia kuwaua. Hii ni kutokana na ukweli kwamba usiku wa kuamkia leo mbwa aina tajwa hapo wamemshambulia mpaka kumuua kijana mtunza bustani ambaye ndo alikuwa akiwatunza na kuwapa chakula.
PAMOJA na kuhitaji kupata ushauri tayari alikuwa ameconclude kuwa Rottweiler siyo mbwa wa kufugwa kitu ambacho mimi na kikataa kutoka na kwamba nimekuwa nikifuga jamii ya mbwa kwa miaka kadhaa, na hata ninapoandika bandiko hili ninao wanne, majike wawili na madume wawili.
JE, NI KWELI KWAMBA ROTTWEILLER NI HATARI SANA?
Jibu ni ndiyo, huyu mbwa anashikilia nafasi ya pili duniani hii ni kwa mjibu wa jarida la K-9 Dog day ya tarehe 26 August 2020, mbwa huyu anaguvu ya kung'ata ( PSI Pound per Square Inch or Pound-force per Square Inch 328 akiwa anakamata nafasi ya 12 dunia. Pamoja na hizo sifa hapo juu mbwa huyu bado kwangu ni mbwa rafiki endapo utakuwa naye karibu na kuonyesha unamjali sana, ( Kifupi ana wivu mnoooo ikiwa ulikuwa umezoea kucheza naye lakini ukabadilika na kuamishia mapenzi kwa kitu kingine kama paka, ng'ombe, mbuzi na hata mtoto Rottweiler anatabia ya kulipa kisasi, hata kama ni wao kwa wao ikiwa wako zaidi ya mmoja na wengine ukawa unawafungia kwenye kennel na mmoja ukamwacha free lazima huyu aliyeko free watamua tu.
Pia kama hauna muda wa kucheza nao kuwatembeza na kuwaruhusu kufanya mazoezi basi usifuge Rottweiler kwani kitakachofuata ni majonzi. Historia ya mbwa huyu inaenda mbali sana tangu zama za ufalme wa kirumi ambapo walitumika kusaidia wafugaji kuchunga mifugo na kuvuta mikokoteni. Kutokana na kuvuta mikokoteni mara nyingi mbwa hawa walivunjika mikia na ndo maana hata leo hii umekuwa kama utamaduni mara nyingi wamiliki wa hawa mbwa huwakata mikia.
NINI UFANYE KAMA UNAFUGA ROTTWEILER
Asubuhi kabla hujawaingiza bandani hakikisha unapata muda wa kuonana nayo cheza nao kidogo wafanyie groomimng, kisha waingize bandani na ikiwa unatabia ya kuwapa breakfast baada ya breakfast waache nje kwa muda ili wacheze, hakikisha una matoyi ya wao kuchezea kama vitenesi ( Napoongelea vitenesi nina maanisha vile ambavyo ni special kwa mbwa usinunue hivi vya kawaida make watatafuna na kumeza na hii inaweza kupelekea kifo. Nunua mifupa ile ya mpira wape waangaike nayo kwa muda kisha warudishe bandani.
Wafundishe utii kwa zile basic command kama ACHA, NJOO, INGIA NDANI. Tumia lugha hiyo kila siku.
KUWA NA MUDA MAALUM WA KUWAPA CHAKULA
Usiwaache na njaa muda mrefu na endapo umechelewa kuwapa chakula na ikawa tayari ni usiku kabla ya kuwafungulia jaribu kuvaa nguo walizozizoea na usijipulizie manukato. Ikiwa umewafungua banda anza na yule mkorofi zaidi akishatoka nje akiwa peke yake ni rahisi kumkontrol na hatimaye kukutambua tena. Baada ya hapo ndo ufungulie waliobaki. Endapo utawafungulia wote na ni usiku wakaona labda paka na kuanza kumfukuza ukijaribu kuwazuia wasiposikia usijaribu kuwapiga make tayari wana hasira na watakugeuka. Wazungu wanesema respect the power' Rottweiler is a loaded gun if not properly handled. Be Leader and not a boss to the breed.
Usiwaache wakuongoze bali uwaongoze ( These are dogs and they leave in packs ) wewe ndo uwe pack leader na si wao.
Usiache hawa mbwa kuhudumiwa na house boy au garderner muda wote, kama itabidi basi mfundishe namna ya kuishi na hawa mbwa.
NAWAPENDA ROTTWEILER
Kwa sababu najihisi salama zaidi kuliko mbwa mwingine yeyote, kwangu mimi wamewahi kumdhibiti mchawi saa nane usiku, na ikabidi yeye mwenyewe aombe msaada na kuonekana na kila mtu pale nyumbani usku.
UFANYE NINI
UKISHAONA MBWA WAKO WANAMSHAMBULIA MTU NDANI YA COMPOUND USITUMIE FIMBO BALI WAZUIE KWA ORDER YA MDOMO NA IKIWA HAWAKUSIKILIZI TUMIA MPIRA KUWA MWAGIA MAJI.
Nasema hivi kwa sababu huyu aliyeuliwa wamiliki na waajiri wameshindwa kumsaidia hii ni kwa sababu hawajawazoea mbwa, wameita kampuni ya ulinzi nayo ikashindwa kumwokoa mpaka polisi nao hakuweza kumwokoa mpaka walipolazimika kupiga mbwa wote wanne risasi. Lakini ikiwa hii kampuni wangejua namna ya kumwokoa mtu anayeshambuliwa na mbwa ilikuwa watume gari ya fire na siyo mobili crews ambao pamoja na bunduki zao hawakuweza kutoa msaada.
Hao sio mbwa aisee, nahisi ndio waliomuondoa Kingunge[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Unawaonyesha kwanza kabla haujaivaa
Nashukuru kwa kuongezea nyama kwa namna navolijua tukio, kujitosa kumwokoa pale ilitakiwa mbinu na si ujasiri. Make wale viumbe walishapata harufu ya damu, hivo yeyote ambaye angeingia kichwa kichwa ilikuwa iwe halali yao.Labda nijaribu kumsaidia mtoa mada sikuwepo eneo la tukio lakini nipo sana jirani na tukio lilipotokea na majirani walinipa dodoso ingawa sikufika,
1. Baba mwenye nyumba hakuwepo nyumbani alikuwa amesafiri siku ya tukio ni mama na kijana wa kazi walikuwepo nyumbani unajua wakina mama wanavyoogopa hawa wanyama.
2. Nikiwa nimelala mida ya saa 7 usiku nilianza kusikia milio ya risasi, kwa uzoefu wangu mdogo wa milio ya risasi nikajua kabisa hiyo ni silaha ndogo bastola less than 9mm, baadae kama saa 7.30 nikaanza kusikia milio ya shortgun hii ni silaha kubwa kidogo ambayo inatumiwa na walinzi wa makampuni binafsi, nikajua ni majambazi na askari wanarushiana risasi nikamwambia masai (mlinzi) wangu akae tayari.
3. Kufikaa saa 8 usiku nikasikia mlio wa SMG (Sub Machine gun) mlio haswa nikasema hili leo balaaa.
4. Nikampigia tena masai wangu mlinzi saa hiyo hiyo akiwa kajificha kichakani anasema pia anasikia sauti ya mtu analia sana , nikajua labda jambazi mmoja kajeruhiwa.
5. Baadae nikapata stori kwamba, baada ya mama mwenye nyumba kushindwa kuwamudu wale mbwa na silaha ndogo, aliwaita walinzi wa makampuni binafsi lakini baada ya kuona lile tukio wale askari wa kampuni binafsi wakasema wao hawawezi tumia short gum kuua wale mbwa kwa sababu risasi za short gun zinasambaa zinaweza mletea madhara yule kijana pia wakachemsha, nahisi walijaribu hata hatuwezi jua labda pia zilimpata, mida kama ya saa 9 kasoro polisi wakaitwa ndio wakaja na SMG wakapiga ule mlio mkubwa niliusikia kuwatawanya mbwa ndio baadae wakawapiga risasi na silaha ndogo.
6. Inaonekana mbwa wale walizoea milio ya silaha ndogo kwa hiyo walikuwa hawashtuki kwa wakati ule
7. Binafsi mimi nafuga mbwa lakini bado sipati picha kama watu wote waliogopa kujitosa kumuokoa yule mtoto pamoja na majirani wakiwepo kushuhudia. Kama unafuga mbwa na unaona huwezi kumcontrol bora uza.
Mbwa mwitu ndio mnyama pori ila Mbwa ni rafiki mkubwa sana wa binadamu ukijua kumhandleHapa navuta picha ningekuwa Ni Mimi ningewapasua vichwa hao makoko wote mmoja mmoja.
Kwamba unakamata mmoja unanyanyua juu na kubwaga chini au kupigiza ukutani.
Ila mnaofuga Hawa wanyamapori sijui huwa mnawaza nini
Huko ni kufuga kifo ndani kwako, kama alivyosema kuwa mbwa hao ni loaded gunHao sio mbwa aisee, nahisi ndio waliomuondoa Kingunge
Napenda sana mbwa na paka ila huyu hata bure simtakiHuko ni kufuga kifo ndani kwako, kama alivyosema kuwa mbwa hao ni loaded gun
Nauliza hivyo nikiwa na sababu mkuu. Kuna jirani yetu aling'atwa na mbwa hao akalazwa hospitali. Hatujui hatma yake ndio nauliza huenda akawa yeye..Siyo lazima Sana kujibu hilo swali mkuu, Samahani
Ni wapi huko mkuu...Hawa mbwa ni hatari kuliko maelezo ....hili tukio lilitokea karibu kabisa na nyumbani kwangu sikulala usiku huo nilianza kusikia milio ya risasi kuanzia saa 7 mpaka saa 9 usiku ya aina mbalimbali ya bunduki nikajua ni majibishano ya risasi ya polisi na majambazi kumbe ni majirani waliojitolea kuuwa mbwa wale lakini wakashindwa mpaka pale askari maalum walipowasili ndio wakafanikiwa kuuwa wale mbwa huku kijana akiwa hoi....kila mtu alikuwa hoi na tukio hili....
Sijawahi experience mbwa wote, ila kwa mujibu Kennel tofauti. Kila Mbwa ana sifa zake. Kwa list ya ubora wote anaanza German Shepherd akifuatiwa na Rottweiler hasa kwa upande wa intelligence na securityHV mnanjua Pitbull nyie...huyo rotywear cha mtoto kabisa
Kabisa hiyo Sura ni kama inasubiri ugomvi maana anaonekana kajaa hasiraMbwa mwenyewe anaonekana amekaa kishari shari tu.
Bora nikomae na hawa hawa kina bobi.Kabisa hiyo Sura ni kama inasubiri ugomvi maana anaonekana kajaa hasira
Bongo Shepherd
Ninaye mungelea hajalazwa mahali popoteNauliza hivyo nikiwa na sababu mkuu. Kuna jirani yetu aling'atwa na mbwa hao akalazwa hospitali. Hatujui hatma yake ndio nauliza huenda akawa yeye..
Kaka swala la silaha ni la ndani, hujaona kesi mtoto anakutwa na silaha ya baba na anafanya nayo tukio, hayo ni mambo ya ndani sana, mke ni mtu wa karibu sana kuwa na silaha yako kulingana na tukio ana haki kisheria kutumia silaha yako kuokoa uhai wa mtu. Hii hata mahakamani anashinda kama ndivyo ilivyokuwaNashukuru kwa kuongezea nyama kwa namna navolijua tukio, kujitosa kumwokoa pale ilitakiwa mbinu na si ujasiri. Make wale viumbe walishapata harufu ya damu, hivo yeyote ambaye angeingia kichwa kichwa ilikuwa iwe halali yao.
Pia hujagusia kipengele kwa nini hawa mbwa wamshambulie huyo ambaye alikuwa anawahudumia?
Swali la kichokozi je mwenye nyumba akisafiri anakambidhi mama bastola?
Hitimisho, nashukuru kwamba nawe umehitimisha kwamba handler alishindwa kucontrol, owner naye kashindwa, kampuni ya ulinzi nayo ikashindwa, mwisho wakaitwa polisi
hivi mnamchukuliaje simba?? hakuna mbwa anayeweza kuua simba.labda au kitoto cha simbaYule mwenye sifa ya kuua hadi Simba ni yupi??