Mbwa jamii ya Rottweiller waua mwangalizi wao Dar

Mbwa jamii ya Rottweiller waua mwangalizi wao Dar

Si ndo hapo sasa...huu ni mfugo au kisanga?

Kwa maelezo ya jamaa hapo juu inaonekana hivi viumbe si vya kufuga Ila binadamu wamelazimisha....eti ukichelewa kuwafungulia vaa nguo walizozoea wakati mi najua Mbwa hutambua Kwa harufu...kuna kitu hakipo sawa hapa.
Hivi hawa mbwa unawajua au unawasikia?!! Ngoja nikwambie kitu anko wangu ambaye ndio owner pamoja na kwamba wanamwogopa na kumtii lakin akijaribu kunyata hata hatua mbili tu yan ni kama vile wameona paka,yan wanamgeukia dk 0 utadhani sio mbwa wake
 
Kwa muda wa miezi kadhaa niliyoishi kwenye nyumba wanayofuga mbwa kadhaa na hao wakiwemo naweza kusema haya kuwahusu Rottweiler. Kwanza kabisa nyumba ina idadi ya mbwa wa ulinzi 7,wa nne ni Rottweiler, mmoja ni German Shepherd (Black),mwingine ni Bull Dog Boerboel.
-Hasa kwa hawaRottweiler kwanza hawapendi makelele,yan kama mbwa next to Rottweiler anabwekabweka hovyo basi ukiwafungulia wakat wa chakula kwanza ataenda kumfunza adabu mbwa aliyekuwa anapiga kelele kabla hajala msosi wake. -Pili wana wivu sana,nakumbuka kuna pet dog wa ndani ni very white so Rottweiler anamchukia sana huyu pet dog cuz the whole family seems to give him much attention than any of the dog na balaa lao hawa mbwa kila siku kabla hawafunguliwa kazi yetu ilikuwa ni kuhakikisha pet dogs wote tumewafungia ndani kabla hawa wengine hawajafunguliwa maana once they are out cha kwanza wanamsaka Rooney na Lola (pet dogs).
-Tatu ni mabondia hawa mbwa. Imagine Bongo (Boerboel) ni mbwa mkubwa sana,ni mzito halafu ana nguvu kwanza ukimwona kwa mara ya kwanza waweza kimbia mbio, hasa pamoja na kwamba ni mkubwa lakn Rottweiler anatembeza kipigo kwa huyu mbwa kama vile mtoto wake despite that sio kwamba ni wakubwa kiivyo ila ndio basi tena ndio wababe kwa mbwa yoyote yule.
-They are serious killer. Narudia tena hawa mbwa ni wauwaji,hawajeruhi bali wanaua kabisa kama wafanyavyo wanyama wakali wa mwituni. Nilishawahi kusoma na kuckia visa mbalimbali vilivyoripoti watoto kuuawa na mbwa hawa.
-They are freaking scary like crazy. Siku moja tupo mitaa ya mikocheni kuwatembeza basi karibia kila gari tunalopishana nalo linatukemea kama vile tumebeba mabomu, wengine wanadiriki kututishia kutushtaki kufanya matembezi mtaani na mbwa huyo,hii inamaanisha hawa mbwa ni very notorious kwa kusababisha maafa pale wasipodhibitiwa ipasavyo.
Ni hayo machache ktk mengi niliyopata kujifunza kuhusu mbwa huyu aina ya Rottweiler. Ikumbukwe kwamba ktk kipind chote hicho sijawahi kukaa nao karibu isipokuwa wale mbwa wengine, i used to observe them from afar but never come into close contact with the freaking Rottweiler. Nawapenda sana mbwa lakn kwa hawa hata sijui nifanyeje maana nawapenda lakn wananitisha sana na wana angalia yao hiyo akikupiga jicho hilo ni bora hata lile la lecturer pale unapocheat.
Bye bye!!!
 
Mbwa kwa ajili ya ulinzi ila sharti na ww umlinde
Mbwa an nana hiyo, atamaliza familia nzima. Yaani, utapigiwa simu labda na majirani kuwa huku kwako mbwa kaleta shida , na ukifia nyumbani unakuta house giril, watoto wote wameliw ana mbwa! Yaani usithubutu kufuga mnyama wa namna hiyo, amabye muda wo wote anateketeza familia, maana akianza na mmoja na atakayekuaj kuokoa naye ataliwa! Bora usiwe na mbwa, Ulinzi wa Mungu unatosha, hizi mbwembwe za kuweka kibao kuna mbwa mkali.. ohh. Nikutafuta kifo kabla ya muda. Hayo wanayaweza Wazungu maana wana adabu ya kutulia nyumbani na hata kufuata hayo masharti lakini kwa wabongo, ni majanga makubwa
 
Mbwa an nana hiyo, atamaliza familia nzima. Yaani, utapigiwa simu labda na majirani kuwa huku kwako mbwa kaleta shida , na ukifia nyumbani unakuta house giril, watoto wote wameliw ana mbwa! Yaani usithubutu kufuga mnyama wa namna hiyo, amabye muda wo wote anateketeza familia, maana akianza na mmoja na atakayekuaj kuokoa naye ataliwa! Bora usiwe na mbwa, Ulinzi wa Mungu unatosha, hizi mbwembwe za kuweka kibao kuna mbwa mkali.. ohh. Nikutafuta kifo kabla ya muda. Hayo wanayaweza Wazungu maana wana adabu ya kutulia nyumbani na hata kufuata hayo masharti lakini kwa wabongo, ni majanga makubwa
Hali mtu bali anauwa tu, kama kula labda ni mtoto mdgo sana. Ikumbukwe kuwa anaua sio kukufanya mtu windo la chakula
 
Kwa ufupi hao mbwa si wakufuga kwa maisha yetu ya Kiswahili, wewe mwenyewe hauli vizuri, mara nyingine hauko nyumbani au ndiyo hivyo huna muda wa kuwaonesha upendo, kwa hoyo, lazima utakaribisha majanga nyumbani. Mfano, unamtoa Kijana wa Kazi huko mkoani alishazoea mbwa wa uswazi ambao anajitafutia chakula mwenyewe na mara nyingi hajulikani yuko wapi. Kwa hiyo, akija mjni na kukutana na mbwa kama ROTTWEILER lazima wataleta majanga kwake au mtu mwingine kwa sababu hatafuata masharti ya namna ya kuwahudumia.
Wawafuge tu! Maana nyumba zetu zenyewe kila mtu anakuja nitaweza wapi kuwalinda hivyo hata mtoto mchanga halindwi hivyo maana unaweza mwacha hapo ukapiga usingizi wako!
 
Wana jamvi niwasalimu kwanza, na moja kwa moja niende kwenye mada.

Asubuhi ya leo nimepokea taarifa toka kwa rafiki yangu mmoja aliyeko Dar akitaka kufahamu kwa nini mbwa jamii ya Rottwieler hugeuka na kushambulia wamiliki na kufikia kuwaua. Hii ni kutokana na ukweli kwamba usiku wa kuamkia leo mbwa aina tajwa hapo wamemshambulia mpaka kumuua kijana mtunza bustani ambaye ndo alikuwa akiwatunza na kuwapa chakula.

PAMOJA na kuhitaji kupata ushauri tayari alikuwa ameconclude kuwa Rottweiler siyo mbwa wa kufugwa kitu ambacho mimi na kikataa kutoka na kwamba nimekuwa nikifuga jamii ya mbwa kwa miaka kadhaa, na hata ninapoandika bandiko hili ninao wanne, majike wawili na madume wawili.

JE, NI KWELI KWAMBA ROTTWEILLER NI HATARI SANA?
Jibu ni ndiyo, huyu mbwa anashikilia nafasi ya pili duniani hii ni kwa mjibu wa jarida la K-9 Dog day ya tarehe 26 August 2020, mbwa huyu anaguvu ya kung'ata ( PSI Pound per Square Inch or Pound-force per Square Inch 328 akiwa anakamata nafasi ya 12 dunia.

Pamoja na hizo sifa hapo juu mbwa huyu bado kwangu ni mbwa rafiki endapo utakuwa naye karibu na kuonyesha unamjali sana, ( Kifupi ana wivu mnoooo ikiwa ulikuwa umezoea kucheza naye lakini ukabadilika na kuamishia mapenzi kwa kitu kingine kama paka, ng'ombe, mbuzi na hata mtoto Rottweiler anatabia ya kulipa kisasi, hata kama ni wao kwa wao ikiwa wako zaidi ya mmoja na wengine ukawa unawafungia kwenye kennel na mmoja ukamwacha free lazima huyu aliyeko free watamua tu.

Pia kama hauna muda wa kucheza nao kuwatembeza na kuwaruhusu kufanya mazoezi basi usifuge Rottweiler kwani kitakachofuata ni majonzi. Historia ya mbwa huyu inaenda mbali sana tangu zama za ufalme wa kirumi ambapo walitumika kusaidia wafugaji kuchunga mifugo na kuvuta mikokoteni. Kutokana na kuvuta mikokoteni mara nyingi mbwa hawa walivunjika mikia na ndo maana hata leo hii umekuwa kama utamaduni mara nyingi wamiliki wa hawa mbwa huwakata mikia.

NINI UFANYE KAMA UNAFUGA ROTTWEILER
Asubuhi kabla hujawaingiza bandani hakikisha unapata muda wa kuonana nayo cheza nao kidogo wafanyie groomimng, kisha waingize bandani na ikiwa unatabia ya kuwapa breakfast baada ya breakfast waache nje kwa muda ili wacheze, hakikisha una matoyi ya wao kuchezea kama vitenesi ( Napoongelea vitenesi nina maanisha vile ambavyo ni special kwa mbwa usinunue hivi vya kawaida make watatafuna na kumeza na hii inaweza kupelekea kifo. Nunua mifupa ile ya mpira wape waangaike nayo kwa muda kisha warudishe bandani.

Wafundishe utii kwa zile basic command kama ACHA, NJOO, INGIA NDANI. Tumia lugha hiyo kila siku.

KUWA NA MUDA MAALUM WA KUWAPA CHAKULA
Usiwaache na njaa muda mrefu na endapo umechelewa kuwapa chakula na ikawa tayari ni usiku kabla ya kuwafungulia jaribu kuvaa nguo walizozizoea na usijipulizie manukato. Ikiwa umewafungua banda anza na yule mkorofi zaidi akishatoka nje akiwa peke yake ni rahisi kumkontrol na hatimaye kukutambua tena. Baada ya hapo ndo ufungulie waliobaki.

Endapo utawafungulia wote na ni usiku wakaona labda paka na kuanza kumfukuza ukijaribu kuwazuia wasiposikia usijaribu kuwapiga make tayari wana hasira na watakugeuka. Wazungu wanesema respect the power' Rottweiler is a loaded gun if not properly handled. Be Leader and not a boss to the breed.

Usiwaache wakuongoze bali uwaongoze (These are dogs and they leave in packs ) wewe ndo uwe pack leader na si wao.
Usiache hawa mbwa kuhudumiwa na house boy au garderner muda wote, kama itabidi basi mfundishe namna ya kuishi na hawa mbwa.

NAWAPENDA ROTTWEILER
Kwa sababu najihisi salama zaidi kuliko mbwa mwingine yeyote, kwangu mimi wamewahi kumdhibiti mchawi saa nane usiku, na ikabidi yeye mwenyewe aombe msaada na kuonekana na kila mtu pale nyumbani usku.

UFANYE NINI
UKISHAONA MBWA WAKO WANAMSHAMBULIA MTU NDANI YA COMPOUND USITUMIE FIMBO BALI WAZUIE KWA ORDER YA MDOMO NA IKIWA HAWAKUSIKILIZI TUMIA MPIRA KUWA MWAGIA MAJI.


Nasema hivi kwa sababu huyu aliyeuliwa wamiliki na waajiri wameshindwa kumsaidia hii ni kwa sababu hawajawazoea mbwa, wameita kampuni ya ulinzi nayo ikashindwa kumwokoa mpaka polisi nao hakuweza kumwokoa mpaka walipolazimika kupiga mbwa wote wanne risasi. Lakini ikiwa hii kampuni wangejua namna ya kumwokoa mtu anayeshambuliwa na mbwa ilikuwa watume gari ya fire na siyo mobili crews ambao pamoja na bunduki zao hawakuweza kutoa msaada.
Kwa haya masharti. Naweza sema ni Bora niachane nao. Mbwa Aina gani anaweza kuwa rafiki wa watu kirahisi??
 
Wakuu habari zenu,
Kuna video nimeiangalia ndani ya dkk 3 mbwa wameua mtu. Nikaukumbuka huu uzi. Msicheze na mbwa majumbani mwa watu, hata ukiona wametulia usiingie mpk mwenyeji aje jmn. Ni hatari
 

Attachments

  • VID-20210813-WA0005.mp4
    1.4 MB
Wakuu habari zenu,
Kuna video nimeiangalia ndani ya dkk 3 mbwa wameua mtu. Nikaukumbuka huu uzi. Msicheze na mbwa majumbani mwa watu, hata ukiona wametulia usiingie mpk mwenyeji aje jmn. Ni hatari
huyo si mwizi wacha aipate fresh yake kabsaaaa
 
Yule mwenye sifa ya kuua hadi Simba ni yupi??
Anatolian Shepherd /Kangal, native country ni Turkey. Kwa Africa, niliwaona Kalkrand, Hardap (Namibia), kuna Jamii za wafugaji wanapakana na mbuga za wanyama hivyo kupelekea ugomvi wa mara kwa mara na watu wa hifadhi.

Simba na chui walikua wanakula mifugo ya wafugaji, wafugaji wakawa wanalipa kisasi kwa kuua simba na chui mbugani.

Kuna mradi ukaleta Anatolian shepherds kwa wafugaji, kwani ni wakubwa na wana uwezo wa kupambana na simba na chui. Lengo ni kusaidia binadamu, mifugo na wanyama pori ku co-exist.
64fcb0da6e5777c0e9b846e4573b6bd3.jpg
7db5c668f4ad754e463fe75867d02d88.jpg
 
Anatolian Shepherd /Kangal, native country ni Turkey. Kwa Africa, niliwaona Kalkrand, Hardap (Namibia), kuna Jamii za wafugaji wanapakana na mbuga za wanyama hivyo kupelekea ugomvi wa mara kwa mara na watu wa hifadhi.

Simba na chui walikua wanakula mifugo ya wafugaji, wafugaji wakawa wanalipa kisasi kwa kuua simba na chui mbugani.

Kuna mradi ukaleta Anatolian shepherds kwa wafugaji, kwani ni wakubwa na wana uwezo wa kupambana na simba na chui. Lengo ni kusaidia binadamu, mifugo na wanyama pori ku co-exist. View attachment 1894930View attachment 1894931
Dah! Kwa hiyo hapo simba anavunjwa mfupa?
 
Dah! Kwa hiyo hapo simba anavunjwa mfupa?
Mfano umeona huyu wa chini amevalishwa "spiked-iron collar" collar ya chuma yenye ncha shingoni , hiyo inamsaidia mbwa pindi ambanapo na wanyama mwitu asidhurike shingo.
7db5c668f4ad754e463fe75867d02d88.jpg
 
Anatolian Shepherd /Kangal, native country ni Turkey. Kwa Africa, niliwaona Kalkrand, Hardap (Namibia), kuna Jamii za wafugaji wanapakana na mbuga za wanyama hivyo kupelekea ugomvi wa mara kwa mara na watu wa hifadhi.

Simba na chui walikua wanakula mifugo ya wafugaji, wafugaji wakawa wanalipa kisasi kwa kuua simba na chui mbugani.

Kuna mradi ukaleta Anatolian shepherds kwa wafugaji, kwani ni wakubwa na wana uwezo wa kupambana na simba na chui. Lengo ni kusaidia binadamu, mifugo na wanyama pori ku co-exist. View attachment 1894930View attachment 1894931
Hakuna mbwa wa kupambana na Simba labda wawe wengi. Akipigwa kofi moja hawezi nyanyuka
 
Back
Top Bottom