Mbwa jamii ya Rottweiller waua mwangalizi wao Dar

Hivi hawa mbwa unawajua au unawasikia?!! Ngoja nikwambie kitu anko wangu ambaye ndio owner pamoja na kwamba wanamwogopa na kumtii lakin akijaribu kunyata hata hatua mbili tu yan ni kama vile wameona paka,yan wanamgeukia dk 0 utadhani sio mbwa wake
 
Kwa muda wa miezi kadhaa niliyoishi kwenye nyumba wanayofuga mbwa kadhaa na hao wakiwemo naweza kusema haya kuwahusu Rottweiler. Kwanza kabisa nyumba ina idadi ya mbwa wa ulinzi 7,wa nne ni Rottweiler, mmoja ni German Shepherd (Black),mwingine ni Bull Dog Boerboel.
-Hasa kwa hawaRottweiler kwanza hawapendi makelele,yan kama mbwa next to Rottweiler anabwekabweka hovyo basi ukiwafungulia wakat wa chakula kwanza ataenda kumfunza adabu mbwa aliyekuwa anapiga kelele kabla hajala msosi wake. -Pili wana wivu sana,nakumbuka kuna pet dog wa ndani ni very white so Rottweiler anamchukia sana huyu pet dog cuz the whole family seems to give him much attention than any of the dog na balaa lao hawa mbwa kila siku kabla hawafunguliwa kazi yetu ilikuwa ni kuhakikisha pet dogs wote tumewafungia ndani kabla hawa wengine hawajafunguliwa maana once they are out cha kwanza wanamsaka Rooney na Lola (pet dogs).
-Tatu ni mabondia hawa mbwa. Imagine Bongo (Boerboel) ni mbwa mkubwa sana,ni mzito halafu ana nguvu kwanza ukimwona kwa mara ya kwanza waweza kimbia mbio, hasa pamoja na kwamba ni mkubwa lakn Rottweiler anatembeza kipigo kwa huyu mbwa kama vile mtoto wake despite that sio kwamba ni wakubwa kiivyo ila ndio basi tena ndio wababe kwa mbwa yoyote yule.
-They are serious killer. Narudia tena hawa mbwa ni wauwaji,hawajeruhi bali wanaua kabisa kama wafanyavyo wanyama wakali wa mwituni. Nilishawahi kusoma na kuckia visa mbalimbali vilivyoripoti watoto kuuawa na mbwa hawa.
-They are freaking scary like crazy. Siku moja tupo mitaa ya mikocheni kuwatembeza basi karibia kila gari tunalopishana nalo linatukemea kama vile tumebeba mabomu, wengine wanadiriki kututishia kutushtaki kufanya matembezi mtaani na mbwa huyo,hii inamaanisha hawa mbwa ni very notorious kwa kusababisha maafa pale wasipodhibitiwa ipasavyo.
Ni hayo machache ktk mengi niliyopata kujifunza kuhusu mbwa huyu aina ya Rottweiler. Ikumbukwe kwamba ktk kipind chote hicho sijawahi kukaa nao karibu isipokuwa wale mbwa wengine, i used to observe them from afar but never come into close contact with the freaking Rottweiler. Nawapenda sana mbwa lakn kwa hawa hata sijui nifanyeje maana nawapenda lakn wananitisha sana na wana angalia yao hiyo akikupiga jicho hilo ni bora hata lile la lecturer pale unapocheat.
Bye bye!!!
 
Mbwa kwa ajili ya ulinzi ila sharti na ww umlinde
Mbwa an nana hiyo, atamaliza familia nzima. Yaani, utapigiwa simu labda na majirani kuwa huku kwako mbwa kaleta shida , na ukifia nyumbani unakuta house giril, watoto wote wameliw ana mbwa! Yaani usithubutu kufuga mnyama wa namna hiyo, amabye muda wo wote anateketeza familia, maana akianza na mmoja na atakayekuaj kuokoa naye ataliwa! Bora usiwe na mbwa, Ulinzi wa Mungu unatosha, hizi mbwembwe za kuweka kibao kuna mbwa mkali.. ohh. Nikutafuta kifo kabla ya muda. Hayo wanayaweza Wazungu maana wana adabu ya kutulia nyumbani na hata kufuata hayo masharti lakini kwa wabongo, ni majanga makubwa
 
Hali mtu bali anauwa tu, kama kula labda ni mtoto mdgo sana. Ikumbukwe kuwa anaua sio kukufanya mtu windo la chakula
 
Wawafuge tu! Maana nyumba zetu zenyewe kila mtu anakuja nitaweza wapi kuwalinda hivyo hata mtoto mchanga halindwi hivyo maana unaweza mwacha hapo ukapiga usingizi wako!
 
Kwa haya masharti. Naweza sema ni Bora niachane nao. Mbwa Aina gani anaweza kuwa rafiki wa watu kirahisi??
 
Wakuu habari zenu,
Kuna video nimeiangalia ndani ya dkk 3 mbwa wameua mtu. Nikaukumbuka huu uzi. Msicheze na mbwa majumbani mwa watu, hata ukiona wametulia usiingie mpk mwenyeji aje jmn. Ni hatari
 

Attachments

  • VID-20210813-WA0005.mp4
    1.4 MB
Wakuu habari zenu,
Kuna video nimeiangalia ndani ya dkk 3 mbwa wameua mtu. Nikaukumbuka huu uzi. Msicheze na mbwa majumbani mwa watu, hata ukiona wametulia usiingie mpk mwenyeji aje jmn. Ni hatari
huyo si mwizi wacha aipate fresh yake kabsaaaa
 
Yule mwenye sifa ya kuua hadi Simba ni yupi??
Anatolian Shepherd /Kangal, native country ni Turkey. Kwa Africa, niliwaona Kalkrand, Hardap (Namibia), kuna Jamii za wafugaji wanapakana na mbuga za wanyama hivyo kupelekea ugomvi wa mara kwa mara na watu wa hifadhi.

Simba na chui walikua wanakula mifugo ya wafugaji, wafugaji wakawa wanalipa kisasi kwa kuua simba na chui mbugani.

Kuna mradi ukaleta Anatolian shepherds kwa wafugaji, kwani ni wakubwa na wana uwezo wa kupambana na simba na chui. Lengo ni kusaidia binadamu, mifugo na wanyama pori ku co-exist.
 
Dah! Kwa hiyo hapo simba anavunjwa mfupa?
 
Dah! Kwa hiyo hapo simba anavunjwa mfupa?
Hahaaa, hapana mkuu, ila hao mbwa wakiwa wengi basi ukubwa wao na ukali wao husaidia kufukuza chui, mbwa mwitu na simba wasisogelee mifugo.
 
Dah! Kwa hiyo hapo simba anavunjwa mfupa?
Mfano umeona huyu wa chini amevalishwa "spiked-iron collar" collar ya chuma yenye ncha shingoni , hiyo inamsaidia mbwa pindi ambanapo na wanyama mwitu asidhurike shingo.
 
Hakuna mbwa wa kupambana na Simba labda wawe wengi. Akipigwa kofi moja hawezi nyanyuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…